Nahumu Utangulizi
NMM

Nahumu Utangulizi

Utangulizi
Kitabu cha Nahumu ni unabii kuhusu kuharibiwa kwa Ninawi, mji mkuu wa Ashuru. Waashuru waliiharibu Samaria katika mwaka wa 722 KK, lakini kwa sababu ya kiburi na udhalimu wao, baadaye waliangamizwa mwaka wa 612 KK. Nahumu anaelezea sababu za kuharibiwa kwa mji wa Ninawi kuwa ibada ya sanamu, ukatili, uuaji, uongo, hila, ushirikina, na ukosefu wa haki. Ni mji uliojaa damu (3:1), na mji kama huu hauwezi kuruhusiwa kudumu.
Wazo Kuu
Utakatifu, haki na nguvu za Mwenyezi Mungu ni msingi wa ujumbe wa kitabu hiki. Mwenyezi Mungu anatawala ulimwengu wote, hata wale ambao hawamtambui. Yeye huweka mipaka ya mataifa, na mataifa yanayokiuka sheria zake yataangamizwa. Hata hivyo, lisha ya haya yote, ujumbe wa tumaini uko wazi. Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa hasira (1:3), na mwema (1:7), na anatoa habari njema kwa wale wanaotaka baraka zake Mwenyezi Mungu badala ya hukumu yake (1:15).
Mwandishi
Nahumu.
Tarehe
Karne ya 7 K.K.
Mgawanyo
• Mwenyezi Mungu na hukumu ya uovu (1:1-15)
• Kuangamizwa kwa Ninawi (2:1-13)
• Dhambi ya Ninawi (3:1-19).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu