Nehemia 7
NMM

Nehemia 7

7
1 # 1Nya 26:12-19; Neh 6:1; 8:9; Za 68:25 Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. 2#Neh 10:23; 2:8; Mit 26:24; 1Fal 18:3#Neh 7:3Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. 3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni
(Ezra 2:1-70)
4 # Mit 1:10; Neh 11:1 Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. 5#Mit 2:6; Rum 11:36; 1Kor 4:7; 2Kor 8:16; Yak 1:17; Ezr 2:1-70Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:
6 # Ezr 2:1-10; 2Nya 36:20 Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 7#1Nya 3:19; Ezr 2:2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):
Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:
8# Ay 13:4; Dan 11:27 wazao wa Paroshi 2,172
9wazao wa Shefatia 372
10wazao wa Ara 652
11wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,818
12wazao wa Elamu 1,254
13wazao wa Zatu 845
14wazao wa Zakai 760
15wazao wa Binui 648
16wazao wa Bebai 628
17wazao wa Azgadi 2,322
18wazao wa Adonikamu 667
19wazao wa Bigwai 2,067
20# Ezr 8:6 wazao wa Adini 655
21wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98
22wazao wa Hashumu 328
23wazao wa Besai 324
24wazao wa Harifu 112
25wazao wa Gibeoni 95
26# 2Sam 23:28; Mwa 35:6; Rut 2; 4 watu wa Bethlehemu na Netofa 188
27# Yos 21:18; Ezr 2:23 watu wa Anathothi 128
28watu wa Beth-Azmawethi 42
29# Yos 18:25-26 watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743
30watu wa Rama na Geba 621
31# 1Sam 13:2; Isa 10:27 watu wa Mikmashi 122
32# Mwa 12:8 watu wa Betheli na Ai 123
33watu wa Nebo 52
34wazao wa Elamu 1,254
35wazao wa Harimu 320
36# Neh 3:2 wazao wa Yeriko 345
37# 1Nya 8:12 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 721
38wazao wa Senaa 3,930
39 # 1Nya 24:7 Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973
40# 1Nya 24:14 wazao wa Imeri 1,052
41# 1Nya 9:12; 24:9 wazao wa Pashuri 1,247
42# 1Nya 24:8; Ezr 10:31 wazao wa Harimu 1,017
43Walawi:
wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia) 74
44 # Neh 11:23 Waimbaji:
wazao wa Asafu 148
45 # 1Nya 9:17 Mabawabu wa malango:
wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 138
46 # Neh 3:26 Watumishi wa Hekalu:#7:46 Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).
wazao wa
Siha, Hasufa, Tabaothi,
47wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,
48wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,
49wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,
50wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,
51wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,
52wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,
53wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
55wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
56wazao wa Nesia na Hatifa.
57 # Mwa 9:25, 26; 1Fal 5:13, 14; 2Nya 2:17, 18 Wazao wa watumishi wa Sulemani:
wazao wa
Sotai, Soferethi, Perida,
58wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
59wazao wa Shefatia, Hatili,
Pokereth-Hasebaimu na Amoni.
60# 1Nya 9:2 Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Sulemani 392
61 # Ezr 2:59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
62wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 642
63 # 2Sam 17:27; 19:31-34; 1Fal 2:7; Ezr 2:61 Na kutoka miongoni mwa makuhani:
wazao wa
Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
64Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 65#Kut 28:30; Neh 8:9; Hes 7:89; 27:18-21Kwa hiyo, mtawala#7:65 Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70). aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.#7:65 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
66Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245. 68Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245 69ngamia 435 na punda 6,720.
70 # Neh 8:9; 10:1 Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000#7:70 Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6. za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani. 71#1Nya 29:7; Ezr 2:69Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu,#7:71 Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172. na mane 2,200#7:71 Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300. za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
72 # Ay 34:10; Kut 25:2 Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.
73 # Za 34:20; Neh 11:20; Kut 23:14-17; Law 23:24-44; Ezr 3:1 Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.
Ezra Asoma Sheria
Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu