Utangulizi
Kitabu cha Nehemia kinaendeleza hadithi iliyoanzishwa na Ezra, na kinazungumzia hali ya maisha katika jumuiya ya waliorejeshwa. Somo kuu la Ezra ni kuwekwa wakfu tena kwa Hekalu: jambo kuu analokazia Nehemia ni kule kujengwa tena kwa kuta za mji wa Yerusalemu. Kitabu kinaanza kwa kuelezea hitaji ambalo Yerusalemu lilikuwa nalo la ulinzi utakaoletwa na ujenzi wa kuta zake. Hii inafuatwa na majadiliano wa jinsi kuta zilivyojengwa licha ya shida kadhaa kutoka kwa Wayahudi wenyewe na pia watu wa nje. Siku ya kitaifa ya kutubu ilitangazwa, na mradi huu ukakamilika.
Wazo Kuu
Somo kuu la kitabu hiki ni ukweli wa kusikitisha kwamba watu ni wagumu wa kujifunza masomo ambayo Mwenyezi Mungu anataka kuwafunza. Waisraeli walipelekwa uhamishoni kwa sababu ya dhambi zao, lakini sasa shida zile zile zilijitokeza tena. Watu walikuwa wakipuuza ibada, maombi, na mafunzo ya Neno la Mungu, bila kutaja ukweli kwamba walikuwa wanatendeana yale yasiyo haki. Lakini katika uvumilivu wake, Mwenyezi Mungu aliendelea kuwatuma wajumbe wake kwao ili kuwapa wokovu na msamaha.
Mwandishi
Nehemia.
Tarehe
Karne ya 5 K.K.
Mgawanyo
• Nehemia awasili Yerusalemu (1:1–2:20)
• Kazi ya kujenga kuta yaanza (1:1–7:3)
• Kusoma kwa sheria na toba ya kitaifa (7:4–10:39)
• Kuweka wakfu kwa kuta, na marekebisho ya Nehemia (11:1–13:31).