Hesabu 2
NMM

Hesabu 2

2
Mpangilio Wa Kambi Za Makabila
1 Bwana aliwaambia Musa na Haruni: 2#Za 74:4; Isa 31:9; Yer 4:21“Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali fulani kutoka kwenye hema, kila mwanaume chini ya alama yake pamoja na bendera ya jamaa yake.”
3 # Hes 6:23; Rut 4:20; 1Nya 2:10; Lk 3:32-33; Hes 10:14 Kwa upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu. 4Kundi lake lina watu 74,600.
5 # Hes 1:8; 10:15 Kabila la Isakari watapiga kambi karibu na Yuda. Kiongozi wa watu wa Isakari ni Nethaneli mwana wa Suari. 6#Hes 26:25Kundi lake lina watu 54,400.
7 # Hes 1:9; 10:16; Mwa 49:13; Kum 33:18 Kabila la Zabuloni litafuata. Kiongozi wa watu wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni. 8Kundi lake lina watu 57,400.
9 # Hes 10:14; Amu 1:1; 1Nya 5:2; Za 78:52 Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kuondoka.
10 # Hes 1:5, 53; Kum 33:6 Kwa upande wa kusini kutakuwa kambi ya makundi ya Reubeni chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Reubeni ni Elisuri mwana wa Shedeuri. 11Kundi lake lina watu 46,500.
12 # Hes 10:19; 1:6 Kabila la Simeoni watapiga kambi karibu na Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Surishadai. 13Kundi lake lina watu 59,300.
14 # Hes 10:20; 1:14 Kabila la Gadi litafuata. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli. 15Kundi lake lina watu 45,650.
16 # Hes 10:18; Mwa 49:3 Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni 151,450. Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka.
17 # Hes 1:50; 10:21; Mdo 4:4; Ebr 8:2; 1Kor 14:40 Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.
18 # Hes 1:10, 53; Mwa 48:20; Yer 31:18-20; Za 80:1; Hos 11:3 Upande wa magharibi kutakuwepo na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi. 19Kundi lake lina watu 40,500.
20 # Mwa 48:20; Hes 1:10 Kabila la Manase litafuata baada ya Efraimu. Kiongozi wa watu wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri. 21Kundi lake lina watu 32,200.
22 # Hes 10:24; 1:11; Za 68:27 Kabila la Benyamini litafuata baada ya Manase. Kiongozi wa watu wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni. 23Kundi lake lina watu 35,400.
24 # Hes 10:22; Za 80:2 Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.
25 # Hes 1:22, 53; 10:25; Kum 32:22 Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai. 26Kundi lake lina watu 62,700.
27 # Hes 1:13; 10:26 Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani. 28Kundi lake lina watu 41,500.
29 # Hes 1:15; 10:27; Mwa 30:8; 49:21; 2Fal 15:29 Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani. 30Kundi lake lina watu 53,400.
31 # Hes 10:25; Yos 6:9 Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni 157,600. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya alama yao.
32 # Hes 1:45; Kut 12:35-37; 38:26 Hawa ndio Waisraeli, wakiwa wamehesabiwa kufuatana na jamaa zao. Wote walio kambini kwa makundi yao ni watu 603,550. 33#Hes 1:47; 26:57-62Hata hivyo, Walawi hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine, kama Bwana alivyomwagiza Musa.
34 # Kut 12:37; Hes 24:2, 9; Isa 45:12 Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu Bwana alichomwamuru Musa. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu