Hesabu 26
NMM

Hesabu 26

26
Kuhesabiwa Watu Mara Ya Pili
1 # Hes 14:37; 25:8 Baada ya hiyo tauni, Bwana akamwambia Musa na Eleazari mwana wa kuhani Haruni, 2#Kut 30:11-16; Hes 1:3; Kut 38:25“Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.” 3#Hes 33:48; Yos 13:22; Hes 22:1; Kum 4:46-49Hivyo Musa na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ng’ambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema, 4#Kut 6:14; 13:3“Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Musa.”
Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri:
5 # Hes 1:20; Mwa 46:8, 9; 1Nya 5:3; Ufu 7:5 Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa:
kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki;
kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;
6 # 1Nya 5:3; Mwa 46:9 kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;
kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.
7Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.
8Mwana wa Palu alikuwa Eliabu, 9#Hes 16:1; 1:16; 16:2; Isa 65:16; Kum 11:6; Hes 27:3; 16:1, 2nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Musa na Haruni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana. 10#Kut 15:12; Hes 16:35, 38; Kut 3:12; Ay 31:3; Za 145:20; Yer 29:22; 2Pet 2:6; Yud 1:7Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo. 11#Kut 6:24; Hes 16:33; Kum 5:9; 24:16; 2Fal 14:6; 2Nya 25:4; Eze 18:20Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.
12 # Mwa 46:10; 1Nya 4:24; Kut 6:15 Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli;
kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini;
kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini;
13 # Mwa 46:10 kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera;
kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
14 # Mwa 46:10; Hes 1:23 Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.
15 # Mwa 46:16 Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni;
kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi;
kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;
16kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni;
kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;
17 # Mwa 46:16 kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi;
kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.
18 # Mwa 30:11; Hes 1:25; Yos 13:24-28 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.
19 # Mwa 38:3; Mwa 38:4; 38:7; Mwa 46:12; 1Nya 2:3 Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.
20 # Mwa 38:5; 38:29; Yos 7:17 Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela;
kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi;
kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.
21 # Mwa 38:29; Rut 4:19; 1Fal 2:9 Wazao wa Peresi walikuwa:
kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;
kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.
22 # Hes 1:27 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.
23 # Mwa 46:13; 49:14 Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola;
kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva;
24 # Mwa 46:13 kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu;
kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.
25 # Mwa 30:18 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.
26 # Hes 1:30; Mwa 46:14; 49:13 Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi;
kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni;
kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli.
27 # Mwa 30:20 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.
28 # Hes 1:32; 36:1; Mwa 41:52; Mwa 46:20; 48:3 Wazao wa Yusufu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:
29 # Hes 1:34; Mwa 50:23; Amu 11:1; Hes 32:39 Wazao wa Manase:
kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi);
kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.
30 # Hes 27:1; 36:1; 1Nya 7:14; Yos 17:2; Amu 6:11; 8:2 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi:
kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri;
kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki;
31kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli;
kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu;
32kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida;
kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi.
33 # Hes 27:1; 36:2; Yos 17:3; 1Nya 7:15; Hes 27:3; 36:11 (Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)
34 # Hes 1:35 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.
35 # Hes 1:32; 1Nya 7:20 Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:
kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela;
kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri;
kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;
36Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela:
kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani.
37 # Hes 1:33; Kum 33:13-17 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500.
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yusufu kwa koo zao.
38 # Mwa 46:21; Hes 1:36; 1Nya 8:40 Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela;
kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli;
kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu;
39 # Mwa 46:21; 1Nya 7:12 kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu;
kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.
40 # Mwa 46:21; 1Nya 8:3 Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa:
kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi;
kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani.
41 # Hes 1:37 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600.
42 # Hes 1:38, 39; Amu 18:19; Mwa 46:23; Mwa 49:16; Kum 33:22 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao:
kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani: 43Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400.
44 # Hes 1:40; 26:47; Hes 1:41 Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna;
kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi;
kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;
45kutoka kwa wazao wa Beria:
kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi;
kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli.
46(Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)
47Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.
48 # Mwa 30:8; Mwa 46:24; 1Nya 7:13 Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli;
kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;
49 # 1Nya 7:13 kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri;
kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.
50 # Hes 1:42, 43 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.
51 # Kut 12:37; Hes 1:46; 2:32 Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730.
52 Bwana akamwambia Musa, 53#Yos 11:23; 14:1; Eze 45:8“Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina. 54#Hes 33:54; 35:8Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa. 55#Hes 34:13; Yos 11:23; 14:2Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao. 56Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”
57 # Mwa 46:11; Kut 6:16; 1Nya 6:16 Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:
kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni;
kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi;
kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.
58 # Kut 6:20 Hizi pia zilikuwa koo za Walawi:
ukoo wa Walibni;
ukoo wa Wahebroni;
ukoo wa Wamahli;
ukoo wa Wamushi;
ukoo wa wana wa Kora.
(Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu; 59#Kut 2:1; 6:20; 2:4; 15:20jina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Haruni, Musa na dada yao Miriamu. 60#Kut 6:23Haruni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari. 61#Law 10:1-2; Hes 3:4; 1Nya 24; 2Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele za Bwana kwa moto usioruhusiwa.)
62 # Hes 3:39; 1:47; 18:23; 2:33; Hes 18:20-24; 35:2-8; Kum 14:27-29 Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.
63 # Hes 1:19; Hes 22:1 Hawa ndio walioorodheshwa na Musa na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko. 64#Hes 14:29; 1:44; Hes 1:1; Kum 2:14, 15Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Musa na kuhani Haruni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai. 65#Hes 14:18; 1Kor 10:5; Hes 13:6; 11:28; Za 90:3-8; Rum 11:22; Kum 32:49-50; Yos 14:10; Hes 14:18, 30; Ebr 3:17, 18; Yud 1:5Kwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu