Hesabu 31
NMM

Hesabu 31

31
Kulipiza Kisasi Juu Ya Wamidiani
1 Bwana akamwambia Musa, 2#Mwa 25:2; Hes 20:26; Hes 25:17; Kum 32:35, 43; Mwa 15:15“Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.”
3 # Amu 11:36; 1Sam 24:12; 2Sam 4:8; 22:48; Za 94:1; 149:7; Isa 34:8; Yer 11:20; 46:10; Eze 25:17; Kum 32:35; Yer 50:28; Za 94:1; Rum 12:19; Ebr 10:30 Kwa hiyo Musa akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi cha Bwana. 4Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.” 5Kwa hiyo waliandaliwa wanaume 12,000 kwa vita, wanaume 1,000 kutoka kila kabila, walitolewa kutoka koo za Israeli. 6#Kut 6:25; Hes 14:44; 10:2; Hes 10:9Musa aliwatuma vitani, watu 1,000 kutoka kila kabila, pamoja na Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, ambaye alichukua vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kuashiria.
7 # Hes 25:16; Kum 20:13; Amu 21:11; 1Fal 11:15; 1Sam 27:9; 1Fal 11:15-16; Kum 20:13; Amu 21:11; Amu 6:2, 33; Amu 6:1 Walipigana dhidi ya Wamidiani, kama Bwana alivyomwagiza Musa, nao waliua kila mwanaume. 8#Yos 13:21; Hes 25:15; 22:5; 24:14; Yos 13:22; Za 9:12; Yud 1:11; Ufu 2:14; 19:20Miongoni mwa watu waliouawa walikuwepo wafalme watano wa Midiani, nao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vilevile walimuua Balaamu mwana wa Beori kwa upanga. 9#Mwa 34:29Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ng’ombe, kondoo na mali zao kama nyara. 10#Yos 6:24; 8:28; 11:11; Amu 18:27; Mwa 25:16; 1Nya 6:54; Za 69:25; Eze 25:4Walichoma moto miji yote ambayo Wamidiani walikuwa wanaishi, pamoja na kambi zao zote. 11#Kum 20:14; 2Nya 28:8Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama, 12#Mwa 49:27; Kut 15:9; Hes 27:2nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Musa na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.
13Musa, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi. 14#Kut 18:21; Kum 1:15; 2Sam 18:1Musa aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.
15 # Kum 2:34; 20:13; Yos 6:21; 8:25; 1Sam 15:3; Yos 10:40; 11:14 Musa akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?” 16#Hes 22:5; 24:14; 2Pet 2:15; Hes 23:25; 25:1-9; 14:37; Yos 22:17; Za 106:28-29; Hos 9:10; Mik 6:5; Ufu 2:14“Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasi Bwana kwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu wa Bwana. 17#Kum 7:2; 20:16; Amu 21:11Sasa waue wavulana wote. Pia muue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa, 18lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.
19 # Hes 5:2; 9:6, 10; 19:11, 12, 16; Law 21:1 “Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu. 20#Hes 19:19; Law 11:32Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”
21Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari waliokuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayo Bwana alimpa Musa: 22#Yos 6:19; 22:8Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi, 23#1Kor 3:13; Hes 8:7; 19:9, 17na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso. 24#Law 11:25; 14:8; Hes 19:10, 22; Za 51:2; Efe 5:26; Ebr 9:9-10Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”
Kugawanya Mateka
25 Bwana akamwambia Musa, 26#Hes 1:4; 1:19“Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa. 27#Yos 22:8; 1Sam 25:13; 30:24; Za 68:12Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya. 28#Hes 18:21; 2Sam 8:11; 1Nya 8:11; 26:27; Isa 18:7; 23:18; Mt 22:21Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya Bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo au mbuzi. 29Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya Bwana. 30#Hes 3:7; 16:3Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Bwana.” 31Kwa hiyo Musa na kuhani Eleazari wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa.
32Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000, 33ng’ombe 72,000, 34punda 61,000, 35na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.
36Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa:
Kondoo 337,500 37#Law 25:23; Kum 10:14; Za 50:12; Mk 12:17; Lk 20:25; 1Kor 10:26ambayo ushuru kwa ajili ya Bwana ilikuwa kondoo 675;
38ng’ombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa ng’ombe 72;
39punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa punda 61;
40Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa watu 32.
41 # Hes 5:9; 18:8, 19 Musa alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Musa.
42Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Musa aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani, 43nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500, 44ng’ombe 36,000, 45punda 30,500, 46na wanadamu 16,000. 47Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Musa alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Bwana.
48Kisha maafisa waliokuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Musa 49#Hes 1:19; Yer 23:4; Kut 23:7; Law 26:7-9; Za 72:14; 116:15; 1Sam 30:19na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana. 50#Kut 30:16; Law 17:11; Mt 20:28; Rum 3:25Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa Bwana vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za Bwana.”
51Musa na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakshiwa. 52Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Musa na kuhani Eleazari walimletea Bwana kama zawadi ilikuwa shekeli 16,750#31:52 Shekeli 16,750 ni sawa na kilo 200. 53#Mwa 34:29; Kum 20:14Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi. 54#Kut 27:21; 40:2; 28:12; Hes 16:40; Kut 30:16; Yos 4:7; Zek 6:14; Lk 22:19; Mdo 1:4Musa na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu