Hesabu 33
NMM

Hesabu 33

33
Vituo Katika Safari Ya Waisraeli
1 # Kut 17:1; 40:36; Hes 1:1; Kut 4:16; 6:26 Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni. 2#Kut 17:4Kwa agizo la Bwana, Musa aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:
3 # Hes 10:2; Mwa 47:11; Yos 5:10; Kut 14:8; Kut 1:11; 12:37; 12:2; 13:4; Za 105:38; Isa 52:12; Kut 14:8 Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 4#Kut 4:23; 2Nya 24:24; Yer 15:3; Eze 14:21; Kut 12:12; Isa 19:1; Sef 2:11; Ufu 12:8waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.
5 # Kut 12:37 Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.
6 # Kut 13:20; Mwa 33:17; Yos 13:27; Za 60:6 Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
7 # Kut 13:17, 18; 14:2, 9 Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
8 # Kut 14:2; 14:22; 15:23 Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.
9 # Kut 15:27 Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.
10 # Kut 16:1 Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.
11 # Kut 16:1; 17:1 Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.
12Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.
13Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.
14 # Kut 15:22; 17:2 Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.
15 # Kut 17:1; 19:1 Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.
16 # Hes 11:34 Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.
17 # Hes 11; 35; Kum 9:22 Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.
18 # Hes 12:16; Kum 1:1 Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.
19Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.
20 # Yos 10:29; 12:15; 15:42; 21:13; 2Fal 8:22; 19:8; 23:31; 1Nya 6:57; 2Nya 21:10; Isa 37:8; Yer 52:1 Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.
21Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.
22Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.
23Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.
24Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.
25Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.
26Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.
27Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.
28Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.
29Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.
30 # Kum 10:6 Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.
31 # Kum 10:6 Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.
32 # Mwa 36:27; Kum 10:6; 1Nya 1:42 Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.
33 # Kum 10:7 Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.
34Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.
35 # Kum 2:8; 1Fal 9:26; 22:48 Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.
36 # Hes 13:21; Hes 20:1; Kum 32:51; Yos 15:1 Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.
37 # Hes 20:22; Mwa 36:16; Hes 20:16 Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. 38#Hes 27:13; Kut 16:35; Hes 20:25-28; Kum 10:6; 32:50Kwa amri ya Bwana, kuhani Haruni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. 39Haruni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.
40 # Mwa 10:18; Hes 21:1; Mwa 12:9; Amu 1:16 Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.
41Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.
42Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.
43 # Hes 21:10 Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.
44 # Hes 21:11 Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.
45 # Hes 32:34 Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.
46 # Yer 48:22; Eze 6:14 Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.
47 # Hes 27:12; 32:3; Kum 32:49 Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.
48 # Hes 27:12; 26:3; Mwa 13:10; Hes 22:1; Yos 12:9 Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko. 49#Yos 12:3; 13:20; Eze 25:9; Hes 21:16Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.
50 # Hes 33:48; 34:2 Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Musa, 51#Kum 7:1; 9:1; Yos 3:17“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani, 52#Law 26:1; Za 106:34-36; Kut 23:24; 34:12-17; Kum 7:2-5, 25, 26; Yos 11:12; 23:7; Amu 2:2wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada. 53#Kum 11:31; 17:14; Yos 1:11; 21:43; Za 24:1; Ay 14:11; Dan 4:35Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki. 54#Law 16:8; Hes 36:2; 26:54; 35:8; Yos 18:10Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.
55 # Yos 23:13; Amu 2:3; Za 106:36; Isa 55:13; Eze 2:6; 28:24; Mik 7:4; 2Kor 12:7; Kut 23:33; Mwa 17:8; Kum 1:7; Za 78:55; 105:11 “ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. 56#Hes 14:28Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu