Utangulizi
Kitabu cha Obadia ni unabii kuhusu kuangamizwa kwa Edomu, taifa ambalo lilijihusisha na kuangamizwa kwa Yerusalemu mnamo 586 K.K. Waedomu walikuwa uzao wa Esau, nao Waisraeli walikuwa uzao wa Yakobo; hao wawili walikuwa ndugu. Edomu wanahukumiwa kwa ukatili wa ndugu (Edomu) dhidi ya ndugu (Israeli). Badala ya kusaidia wakati adui walivamia Israeli, Edomu walisaidia kuangamiza, na pia kuteka nyara mji ulioshindwa.
Wazo Kuu
Ukatili wa Edomu na kiburi chao zilivutia hukumu ya Mwenyezi Mungu. Lengo la Obadia analotaka tuone ni jinsi Mwenyezi Mungu anachukia dhambi. Ya kwamba Mwenyezi Mungu angesimama kando wakati ndugu aliangalia ndugu akiangamizwa, na hata ndugu akasaidia katika mauaji, ni jambo lisilowezekana. Lakini Mwenyezi Mungu aliingilia kati na kuhukumu taifa la Edomu na hatimaye likaangamizwa pia.
Mwandishi
Obadia.
Tarehe
Karne ya 6 K.K.
Mgawanyo
• Kuangamizwa kwa Edomu kwatabiriwa (1-9)
• Dhambi za Edomu (10-14)
• Siku ya Bwana, na kurejezwa kwa Yuda (15-21).