Utangulizi
Onesimo alikuwa mtumwa aliyetoroka kutoka kwa bwana wake Filemoni huko Kolosai, akaenda Rumi. Akiwa humo alisikia Injili kutoka kwa Paulo na akawa muumini. Paulo alimwandikia Filemoni kumshawishi amkubali Onesimo kurudi kwake, wakati huu akiwa zaidi ya mtumwa, bali pia ndugu Mkristo. Katika aya ya 11 Paulo anasema kwamba sasa Onesimo, ambaye jina lake maana yake ni “Mwenye umuhimu,” kwa kweli atakuwa Mwenye umuhimu kwa Filemoni na pia katika huduma.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kifupi kina umuhimu katika njia nyingi. Mambo mawili yanajitokeza: (1) Tunaona jinsi ambavyo Injili ilifanya kazi. Hakuna yeyote, hata mtumwa aliyetoroka, yuko juu ya kazi ya Mwenyezi Mungu. Kama mtu atamwamini Al-Masihi, basi atakuwa mtu mpya. (2) Vikwazo vya zamani vya chuki itokanayo na hadhi ya mtu katika jamii vinavunjwa na Injili, kwani Filemoni na Onesimo sasa ni ndugu Wakristo. Baada ya siku nyingi, mfumo mwovu wa utumwa utaanguka kutokana na uzito wa mafundisho ya Ukristo.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mwaka wa 60 au 61 B.K.
Mgawanyo
• Salamu za Paulo kwa Filemoni (1-3)
• Paulo kumsifu Filemoni (4-7)
• Paulo kumwombea Onesimo (8-21)
• Maneno ya mwisho (22-25).