Wafilipi 1
NMM

Wafilipi 1

1
Salamu
1 # Mdo 16:1; 2Kor 1:1; Mdo 9:13; Mdo 16:12; 1Tim 3:1; 1Tim 3:8 Waraka wa Paulo na Timotheo, watumishi wa Al-Masihi Isa:
Kwa watakatifu wote katika Al-Masihi Isa walioko Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi:
2 # Rum 1:7; 1Kor 1:2; 1Pet 1:2 Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi.
Shukrani Na Maombi
3 # Rum 1:8; 1Kor 1:6, 8; Efe 1:15, 16; 1Kor 1:4; Kol 1:3; 1The 1:2 Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi. 4#Rum 1:10Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, 5#Mdo 2:42; Flp 4:15; Mdo 16:12-40kwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. 6#Flp 2:13; 1Kor 16:8; Za 138:8Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Al-Masihi Isa.
7 # 2Pet 1:13; 2Kor 7:3; Flp 1:13, 14, 17; Mdo 21:33 Ni haki na ni wajibu wangu kufikiri hivi juu yenu nyote, kwa sababu ninyi mko moyoni mwangu. Ikiwa nimefungwa au nikiwa ninaitetea na kuithibitisha Injili, ninyi nyote mnashiriki neema ya Mungu pamoja nami. 8#Rum 1:9; 2Kor 1:23; 1The 2:5Mungu ni shahidi wangu jinsi ninavyowaonea shauku ninyi nyote kwa huruma ya Al-Masihi Isa.
9 # 1The 3:12 Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, 10#1Kor 1:8; Rum 2:18; Efe 5:10; Mdo 24:16; 1The 3:13; 5:23ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Al-Masihi, 11#Yak 3:18; Yn 15:4; Efe 2:10; Kol 1:16; Yn 15:8; Efe 1:12, 14mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Isa Al-Masihi, kwa utukufu na sifa za Mungu.
Kufungwa Kwa Paulo Kwaieneza Injili
12 # 2Tim 2:9 Basi, ndugu zangu, nataka mjue kwamba mambo yale yaliyonipata kwa kweli yamesaidia sana kueneza Injili. 13#Mdo 21:33Matokeo yake ni kwamba imejulikana wazi kwa walinzi wote wa jumba la kifalme na kwa wengine wote kuwa nimefungwa kwa ajili ya Al-Masihi. 14#Mdo 21:33Kwa sababu ya vifungo vyangu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu kwa ujasiri zaidi na bila woga.
15 # Flp 2:3 Ni kweli kwamba wengine wanamhubiri Al-Masihi kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana, lakini wengine wanamhubiri Al-Masihi kwa nia njema. 16#Flp 1:7, 12Hawa wa mwisho wanamhubiri Al-Masihi kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba nimo humu gerezani kwa ajili ya kuitetea Injili. 17#Flp 2:3; Mdo 21:33Hao wa kwanza wanamtangaza Al-Masihi kutokana na tamaa zao wenyewe wala si kwa moyo mweupe, bali wanakusudia kuongeza mateso yangu katika huku kufungwa kwangu. 18#Flp 2:17, 18Lakini inadhuru nini? Jambo la muhimu ni kwamba kwa kila njia, ikiwa ni kwa nia mbaya au njema, Al-Masihi anahubiriwa. Nami kwa ajili ya jambo hilo ninafurahi.
Naam, nami nitaendelea kufurahi, 19#2Kor 1:11; Mdo 16:7; Mdo 16:23kwa maana ninajua kwamba kwa maombi yenu na kwa msaada unaotolewa na Roho wa Isa Al-Masihi, yale yaliyonipata mimi yatageuka kuwa wokovu wangu. 20#Rum 8:19; 1Kor 6:20; Rum 14:8Ninatarajia kwa shauku kubwa na kutumaini kwamba sitaaibika kwa njia yoyote, bali nitakuwa na ujasiri wa kutosha ili sasa kama wakati mwingine wowote, Al-Masihi atukuzwe katika mwili wangu, ikiwa ni kwa kuishi au kwa kufa. 21#Gal 2:20Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Al-Masihi, na kufa ni faida. 22#Rum 1:13Kama nitaendelea kuishi katika mwili, kwangu hili ni kwa ajili ya matunda ya kazi. Lakini sijui nichague lipi? Mimi sijui! 23#2Tim 4:6; Yn 12:26; 2Kor 5:8Ninavutwa kati ya mambo mawili: Ninatamani kuondoka nikakae pamoja na Al-Masihi, jambo hilo ni bora zaidi. 24Lakini kwa sababu yenu ni muhimu zaidi mimi nikiendelea kuishi katika mwili. 25#Flp 2:24Kwa kuwa nina matumaini haya, ninajua kwamba nitaendelea kuwepo na kuwa pamoja nanyi nyote, ili mpate kukua na kuwa na furaha katika imani. 26#2Kor 1:14; 5:12Ili kwamba furaha yenu iwe nyingi katika Al-Masihi Isa kwa ajili yangu kwa kule kuja kwangu kwenu tena.
Kuenenda Ipasavyo Injili
27 # Efe 4:1; 1Kor 16:13; Yud 3 Lakini lolote litakalotukia, mwenende kama ipasavyo Injili ya Al-Masihi, ili kwamba nikija na kuwaona au ikiwa sipo, nipate kusikia haya juu yenu: Kuwa mnasimama imara katika roho moja, mkiishindania imani ya Injili kwa umoja, 28#2The 1:5; Rum 8:17; 2Tim 2:11wala msitishwe na wale wanaowapinga. Hii ni ishara kwao kuwa wataangamia, lakini ninyi mtaokolewa, na hii ni kazi ya Mungu. 29#Mt 5:11, 12; Mdo 5:41; Mdo 14:22Kwa maana mmepewa kwa ajili ya Al-Masihi, si kumwamini tu, bali pia kuteswa kwa ajili yake, 30#Kol 2:1; Ebr 10:32; Mdo 16:19-40kwa kuwa mnashiriki mashindano yale yale mliyoyaona nikiwa nayo na ambayo hata sasa mnasikia kuwa bado ninayo.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu