17
1 #
Mit 15:16, 17; 16:8 Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu
kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.
2 #
Mit 10:5; 19:26 Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye,
naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.
3 #
Mit 27:21; Yer 17:10; 1Pet 1:7; Za 26:2 Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu,
bali Bwana huujaribu moyo.
4Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya;
mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.
5 #
Mit 14:31; Ay 31:39; Eze 25:3; Oba 1:12 Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake;
yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.
6 #
Za 125:5; Mit 13:22 Wana wa wana ni taji la wazee,
nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
7 #
Mit 16:10
Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu:
je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!
8 #
Mwa 39:21; Dan 6:3 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;
kokote kigeukiapo, hufanikiwa.
9 #
Mit 10:12; 16:28 Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo,
bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu.
10Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua
kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.
11Mtu mbaya hupenda kuasi tu;
mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake.
12 #
1Sam 25:25
Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyang’anywa watoto wake,
kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.
13 #
Yer 18:20; 1Sam 19:4; Rum 12:17; Za 109:4-5 Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema,
kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.
14 #
Mit 20:3; Mt 5:25-26; Mdo 6:1 Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji;
kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.
15 #
Za 94:21; Kut 23:6-7; Mit 18:5; Mao 3:34-36; Isa 5:23 Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki,
naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki:
Bwana huwachukia sana wote wawili.
16 #
Mit 23:23
Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu,
wakati yeye hana haja ya kupata hekima?
17 #
2Sam 15:21; Mit 27:10 Rafiki hupenda wakati wote
naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.
18 #
Mit 6:1-5; 11:5 Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani,
naye huweka dhamana kwa jirani yake.
19Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi;
naye ainuaye sana lango lake#17:19 Kuinua lango maana yake ni kusema kwa majivuno. hutafuta uharibifu.
20Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa;
naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.
21 #
Mit 10:1
Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni;
hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.
22 #
Kut 12:46; Za 22:15 Moyo wenye furaha ni dawa nzuri,
bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.
23 #
Kut 18:21; 1Sam 8:3 Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri
ili kupotosha njia ya haki.
24 #
Ay 31:1; Mhu 2:14 Mtu wa ufahamu huitazama hekima,
lakini macho ya mpumbavu huhangaika
hadi kwenye miisho ya dunia.
25 #
Mit 10:1
Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake
na uchungu kwa yeye aliyemzaa.
26 #
Za 94:21; Mit 18:5 Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia,
au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao.
27 #
Ay 6:24; Mit 14:29 Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia,
naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.
28 #
Ay 2:13; Mit 10:19 Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza,
na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.