Mithali 19
NMM

Mithali 19

19
1 # Mit 28:6 Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama,
kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.
2 # Hos 4:6; Yn 16:3; Rum 10:2 Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa,
wala kufanya haraka na kuikosa njia.
3 # Mit 14:1; 9:13; 24:9; Isa 32:6; Yak 1:13-15 Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake
hata hivyo moyo wake humkasirikia Bwana.
4 # Mit 19:7; 14:20 Mali huleta marafiki wengi,
bali rafiki wa mtu maskini humwacha.
5 # Kut 23:1; Kum 19:19; Mit 1:28 Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo hataachwa huru.
6 # Mit 29:26; Mit 17:8; 18:16 Wengi hujipendekeza kwa mtawala
na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi.
7 # Mit 10:15 Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote:
Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani!
Ingawa huwafuata kwa kuwasihi,
hawapatikani popote.
8 # Mit 16:20 Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe,
yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.
9 # Kum 19:19 Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo ataangamia.
10 # Mit 26:1; 30:21-23; Mhu 10:5-7 Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa,
itakuwa vibaya kiasi gani
kwa mtumwa kuwatawala wakuu.
11 # 2Fal 5:12; Mit 16:32; Mt 25:21; Efe 4:32 Hekima ya mtu humpa uvumilivu,
ni kwa utukufu wake kusamehe makosa.
12 # Za 33:3; 72:5-6; Es 1:12 Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba,
bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.
13 # Mit 10:1; Es 1:18; Mit 21:9 Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye,
naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.
14 # 2Kor 12:14; Mit 18:22 Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi,
bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.
15 # Mit 10:4; 20:13 Uvivu huleta usingizi mzito,
naye mtu mzembe huona njaa.
16 # Mit 16:17; Lk 10:28; Rum 2:7 Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake,
bali yeye anayezidharau njia zake atakufa.
17 # Kum 24:19; Mt 10:42; 2Kor 9:6 Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana,
naye atamtuza kwa aliyotenda.
18 # Mit 13:24; 23:13-14 Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini,
usiwe mshirika katika mauti yake.
19Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake,
kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena.
20 # Mit 4:1; 12:15 Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho,
nawe mwishoni utakuwa na hekima.
21 # Es 9:25; Mhu 7:29; Yer 4:29; Mao 3:37; Ebr 6:17 Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,
lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.
22Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,
afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.
23 # Za 25:13; 1Tim 4:8; Ay 4:7; Mit 10:27 Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima,
kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika,
bila kuguswa na shida.
24 # Mit 26:15 Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,
lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!
25 # Za 141:5; Mit 9:9; 21:11 Mpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara,
mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa.
26 # Mit 28:24 Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake
ni mwana aletaye aibu na fedheha.
27 # Mt 7:15; Mk 4:24; Efe 4:14 Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho,
utatangatanga mbali na maneno ya maarifa.
28 # Ay 15:16 Shahidi mla rushwa hudhihaki hukumu
na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi.
29 # Kum 25:2; Mit 26:3 Adhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka
na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu