Mithali 20
NMM

Mithali 20

20
1 # Law 10:9; Hab 2:5; 1Sam 25:36; 1Fal 20:16; Mit 31:4 Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi;
yeyote apotoshwaye navyo hana hekima.
2 # Mit 8:36; 19:12; Es 7:7 Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;
yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake.
3 # Mwa 13:8; Mit 17:14 Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi,
bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.
4 # Mit 6:6; Mhu 10:18 Mvivu halimi kwa majira;
kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama
lakini hapati chochote.
5 # Za 18:16 Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina,
lakini mtu mwenye ufahamu huyachota.
6 # Za 12:1; Mt 6:2; Mhu 7:28; Lk 18:8 Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma,
bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?
7 # Za 26:1; 37:25-26; 112:2 Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,
wamebarikiwa watoto wake baada yake.
8 # 1Fal 7:7; Mit 25:4-5 Wakati mfalme aketipo katika kiti chake cha enzi kuhukumu,
hupepeta ubaya wote kwa macho yake.
9 # Mhu 7:20; 1Fal 8:46; 1Yn 1:8 Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi;
mimi ni safi na sina dhambi?”
10 # Mit 20:23; Mit 11:1 Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti,
Bwana huchukia vyote viwili.
11 # Za 39:1; Mt 7:16 Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,
kama tabia yake ni safi na adili.
12 # Kut 4:11; Rum 11:26; Za 94:9 Masikio yasikiayo na macho yaonayo,
Bwana ndiye alivifanya vyote viwili.
13 # Mit 6:11; 19:15; Rum 12:11 Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini,
uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.
14“Haifai, haifai!” asema mnunuzi,
kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.
15 # Ay 28:12, 16, 17, 18, 19 Dhahabu kunayo, na marijani kwa wingi,
lakini midomo inenayo maarifa
ni kito cha thamani kilicho adimu.
16 # Kut 22:26; Mit 27:13 Chukua vazi la yule awekaye dhamana
kwa ajili ya mgeni;
lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo
kwa ajili ya mwanamke mpotovu.
17Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu,
bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe.
18 # Mit 11:14; 24:6 Fanya mipango kwa kutafuta mashauri,
ukipigana vita, tafuta maelekezo.
19 # Mit 11:13 Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika,
kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi.
20 # Kut 21:17; Mit 30:11; Ay 18:5; Law 20:9 Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake,
taa yake itazimwa katika giza nene.
21 # Mit 28:8; Hab 2:6 Urithi upatikanao haraka mwanzoni,
hautabarikiwa mwishoni.
22 # Mit 24:29; Yer 42:11; Kum 32:35; Rum 12:17-19 Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!”
Mngojee Bwana, naye atakuokoa.
23 # Kum 25:13 Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu,
nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.
24 # Mit 19:21; Yer 10:23; Rum 8:26 Hatua za mtu huongozwa na Bwana.
Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?
25 # Mhu 5:2-5; Yer 44:25 Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka
na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.
26 # Mit 20:8 Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu,
hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.
27 # Za 119:105; Mit 16:2 Taa ya Bwana huchunguza roho ya mwanadamu,
huchunguza utu wake wa ndani.
28 # Mit 29:14; Isa 16:5 Upendo na uaminifu humweka mfalme salama,
kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama.
29 # Mit 16:31 Utukufu wa vijana ni nguvu zao,
mvi ni fahari ya uzee.
30 # Za 51:2; Mit 22:15 Mapigo na majeraha huusafisha ubaya,
nayo michapo hutakasa utu wa ndani.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu