21
1 #
Es 5:1; Yer 39:11-12 Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana;
huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo.
2 #
Mit 24:12; Lk 16:15; Yer 17:10; 1Sam 16:7 Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake,
bali Bwana huupima moyo.
3 #
Hos 6:6; Mik 6:6-8 Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika
zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.
4 #
Ay 41:34; Mit 6:17 Macho ya kudharau na moyo wa kiburi,
ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi!
5 #
Mit 10:4
Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida,
kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini.
6 #
Mit 10:2; 2Pet 2:3 Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo
ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha.
7 #
Mit 11:5
Jeuri ya waovu itawaburuta mbali,
kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa.
8 #
Mit 2:15
Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu,
bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu.
9 #
Mit 21:19; 19:13; 25:24 Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba,
kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.
10 #
Yak 4:5
Mtu mwovu hutamani sana ubaya,
jirani yake hapati huruma kutoka kwake.
11 #
Mit 19:25
Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa,
mjinga hupata hekima;
wakati mtu mwenye hekima afundishwapo,
hupata maarifa.
12 #
1Kor 10:10; Rum 2:8; Mit 14:11 Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu,
naye atawaangamiza waovu.
13 #
Ay 29:12; Zek 7:11; Mdo 7:57; Yak 2:13 Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini,
yeye pia atalia, wala hatajibiwa.
14 #
Mwa 32:20; Mit 18:16 Zawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira
na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali.
15 #
Mit 21:9
Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki,
bali kitisho kwa watenda mabaya.
16 #
Za 49:14; Eze 18:24 Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu,
hupumzika katika kundi la waliokufa.
17 #
Mit 23:20-21, 29-35 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini,
yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri.
18 #
Isa 43:3-4; Mit 11:8 Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki,
nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu.
19 #
Mit 21:9
Ni afadhali kuishi jangwani
kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi.
20 #
Za 112:3; Mit 10:22; Mt 25:3 Katika nyumba ya mwenye hekima
kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta,
lakini mtu mpumbavu
hutafuna vyote alivyo navyo.
21 #
1Kor 15:58; Za 25:13; Mt 5:6 Yeye afuatiaye haki na upendo
hupata uzima, mafanikio na heshima.
22 #
Mit 8:14; Mhu 9:15-16 Mtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu,
na kuangusha ngome wanazozitegemea.
23 #
Za 34:13; Yak 3:2; Mit 12:13 Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake
hujilinda na maafa.
24 #
Yer 43:2
Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake;
hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi.
25 #
Mit 13:4
Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake,
kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.
26 #
Law 25:35; Mt 5:42 Mchana kutwa hutamani zaidi,
lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.
27 #
1Fal 14:24; Amo 5:22; Mit 15:8 Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo,
si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya!
28 #
Isa 29:21; Mit 19:5 Shahidi wa uongo ataangamia,
bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu.
29 #
Mit 14:8
Mtu mwovu ana uso wa ushupavu,
bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake.
30 #
Ay 12:13; Yer 9:23; 2Nya 13:12; Mdo 5:39 Hakuna hekima, wala akili, wala mpango
unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana.
31 #
Isa 31:1; Za 3:8 Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita,
bali ushindi huwa kwa Bwana.