Mithali 22
NMM

Mithali 22

22
1 # Mhu 7:1 Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi,
kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu.
2 # Ay 31:15; Mt 5:45; Za 49:1-2 Tajiri na maskini wanafanana kwa hili:
Bwana ni Muumba wao wote.
3 # Mit 14:16; 27:12; Isa 26:20 Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,
bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa.
4 # Mit 15:33; Mit 10:27; Dan 4:36 Unyenyekevu na kumcha Bwana
huleta utajiri, heshima na uzima.
5 # Mit 15:19; 1Yn 5:18 Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego,
bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo.
6 # Efe 6:4 Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,
naye hataiacha hata akiwa mzee.
7 # Yak 2:6 Matajiri huwatawala maskini
naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.
8 # Hos 10:13; 8:7; Kut 1:20; Gal 6:7-8; Za 125:3 Yeye aupandaye uovu huvuna taabu,
nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa.
9 # Kum 14:29; 2Kor 9:6; Mit 11:25; 28:27 Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa
kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.
10 # Mit 26:20; Mwa 21:9, 10; Za 101:5 Mfukuze mwenye dhihaka,
na mvutano yatatoweka;
ugomvi na matukano vitakoma.
11 # Mit 16:13; Mt 5:8 Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema,
mfalme atakuwa rafiki yake.
12Macho ya Bwana hulinda maarifa,
bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu.
13 # Mit 26:13 Mvivu husema, “Yuko simba nje!”
au, “Nitauawa katika mitaa!”
14 # Mit 6:12; Mhu 7:26 Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu;
yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana
atatumbukia ndani yake.
15 # Mit 13:24; 20:30 Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,
bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.
16 # Ay 20:19-23; Amo 2:6-8; Isa 3:14-15; Yak 2:13 Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali,
naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini.
Misemo Ya Wenye Hekima
17 # Mit 1:8; 1:6; 30:1; 31:1; Mit 2:2 Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima,
elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo,
18kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako
na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako.
19Ili tumaini lako liwe katika Bwana,
hata wewe, ninakufundisha leo.
20 # Mit 8:6 Je, sijakuandikia misemo thelathini,
misemo ya mashauri na maarifa,
21 # 1Pet 3:15; Mhu 12:10 kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika,
ili uweze kutoa majibu sahihi
kwake yeye aliyekutuma?
22 # Law 25:17; Zek 7:10; Kut 23:6; Mal 3:5 Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini,
wala kumdhulumu mhitaji mahakamani,
23 # Ay 29:16; Za 12:5; 1Sam 25:39 kwa sababu Bwana atalichukua shauri lao
naye atawateka wao waliowateka.
24Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka,
usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika,
25 # 1Kor 15:33 la sivyo utajifunza njia zake
na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.
26 # Kum 19:14; Mit 23:10 Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani,
au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni.
27 # Mit 11:15; 17:18 Kama ukikosa njia ya kulipa,
kitanda chako
kitachukuliwa ukiwa umekilalia.
28 # Kum 19:14 Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani
lililowekwa na baba zako.
29 # 1Fal 11:28; Mwa 41:46; Mhu 9:10 Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake?
Atahudumu mbele ya wafalme;
hatahudumu mbele ya watu duni.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu