23
1Uketipo kula chakula na mtawala,
angalia vyema kile kilicho mbele yako,
2na utie kisu kooni mwako
kama ukiwa mlafi.
3 #
Za 141:4
Usitamani vyakula vyake vitamu
kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.
4 #
Yn 6:27; 1Tim 6:9; Rum 12:16 Usijitaabishe ili kuupata utajiri,
uwe na hekima kuonyesha kujizuia.
5 #
Mt 6:19; Mit 27:24 Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka,
huwa kama umepata mabawa ghafula,
ukaruka na kutoweka angani kama tai.
6 #
Za 141:4; Kum 15:9 Usile chakula cha mtu mchoyo,
usitamani vyakula vyake vitamu,
7 #
Za 12:2
kwa maana yeye ni aina ya mtu
ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama.
Anakuambia, “Kula na kunywa,”
lakini moyo wake hauko pamoja nawe.
8Utatapika kile kidogo ulichokula,
nawe utakuwa umepoteza bure
maneno yako ya kumsifu.
9 #
Mit 9:7
Usizungumze na mpumbavu,
kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako.
10 #
Kum 19:14; Mit 22:28 Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani
wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima,
11 #
Ay 19:25; Kut 22:22-24; Yer 50:34; Mit 15:25 kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu,
atalichukua shauri lao dhidi yako.
12 #
Mit 2:2
Elekeza moyo wako kwenye mafundisho
na masikio yako kwenye maneno ya maarifa.
13 #
Mit 13:24; 19:18; 22:18; 22:15; 29:15, 16 Usimnyime mtoto adhabu,
ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa.
14 #
Mit 13:24; 19:18 Mwadhibu kwa fimbo
na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini#23:14 Mautini maana yake ni Kuzimu.
15 #
Mit 23:24, 25; 29:3 Mwanangu, kama moyo wako una hekima,
basi moyo wangu utafurahi,
16 #
Mit 23:24
utu wangu wa ndani utafurahi,
wakati midomo yako
itakapozungumza lililo sawa.
17 #
Za 73:3; Mit 28:14 Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi,
bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana.
18 #
Za 37:1-4; Mit 24:14-20 Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako,
nalo taraja lako halitakatiliwa mbali.
19 #
Kum 4:9; Mit 28:7 Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima,
weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa.
20 #
Hab 2:15; Rum 13:13; Isa 5:22 Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo,
au wale walao nyama kwa pupa,
21 #
Mit 21:17; 19:23; 19:15 kwa maana walevi na walafi huwa maskini,
nako kusinzia huwavika matambara.
22 #
Law 19:32; Efe 6:1-2 Msikilize baba yako, aliyekuzaa,
wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.
23 #
Mit 4:7; 17:16; Mt 13:44 Nunua kweli wala usiiuze,
pata hekima, adabu na ufahamu.
24 #
Mit 23:15-16; Mit 10:1; 15:20 Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa,
naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.
25 #
Mit 10:1
Baba yako na mama yako na wafurahi,
mama aliyekuzaa na ashangilie!
26 #
Mit 5:1-6; Za 18:21 Mwanangu, nipe moyo wako,
macho yako na yafuate njia zangu,
27 #
Mit 22:14
kwa maana kahaba ni shimo refu
na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba.
28 #
Mit 7:11-12; Mhu 7:26 Kama mnyang’anyi, hungojea akivizia,
naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume.
29 #
1Fal 20:16; Mit 20:1; Isa 5:11; Nah 1:10; Mt 24:49, 50; Efe 5:18 Ni nani mwenye ole?
Ni nani mwenye huzuni?
Ni nani mwenye ugomvi?
Ni nani mwenye malalamiko?
Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu?
Ni nani mwenye macho mekundu?
30 #
Za 75:8; Efe 5:18; Mit 20:1; Efe 5:18; Za 75:8; Mit 9:2 Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo,
hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.
31Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu,
wakati unapometameta kwenye bilauri,
wakati ushukapo taratibu!
32Mwishowe huuma kama nyoka
na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.
33Macho yako yataona mambo mageni
na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka.
34Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari,
alalaye juu ya kamba ya merikebu.
35 #
Mit 27:22; Yer 5:3; Kum 29:19; Isa 56:12; 2Pet 2:22 Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia!
Wamenichapa, lakini sisikii!
Nitaamka lini
ili nikanywe tena?”