24
1 #
Mit 3:31-32; 23:17-18 Usiwaonee wivu watu waovu,
usitamani ushirika nao;
2 #
Za 2:1; 10:7; Isa 32:6; 55:7-8; 59:7; 65:2; Hos 4:1 kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri,
nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara.
3 #
Mit 14:1
Kwa hekima nyumba hujengwa,
nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa
4 #
Mit 8:21
kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa
vitu vya thamani na vya kupendeza.
5 #
Mit 21:22
Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa,
naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu,
6 #
Mit 11:14; Lk 14:31 kwa kufanya vita unahitaji uongozi
na kwa ushindi washauri wengi.
7 #
Za 10:5; Mit 14:6 Hekima i juu mno kwa mpumbavu,
katika kusanyiko langoni
hana lolote la kusema.
8 #
Rum 1:30
Yeye apangaye mabaya
atajulikana kama mtu wa hila.
9 #
Mwa 6:5; Za 119:113; Mt 9:4; Mdo 8:22; 2Kor 10:5 #
Mwa 6:5; Mdo 8:22; 2Kor 10:5 Mipango ya upumbavu ni dhambi,
watu huchukizwa na mwenye dhihaka.
10 #
Yer 51:46; Ebr 12:3 Ukikata tamaa wakati wa taabu,
jinsi gani nguvu zako ni kidogo!
11 #
Isa 58:6-7; 1Yn 3:16; Za 82:4 Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo;
wazuie wote wanaojikokota
kuelekea machinjoni.
12 #
Za 139:2; Mit 16:24; 21:2; Yer 32:19; Mt 16:24 Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,”
je, yule apimaye mioyo halitambui hili?
Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili?
Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?
13 #
Wim 5:1
Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri;
asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja.
14 #
Za 119:103; Mit 16:24; 23:18 Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako,
kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo,
nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.
15 #
Za 10:9, 10 Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia
makao ya mwenye haki,
wala usiyavamie makazi yake,
16 #
Ay 5:19; Mik 7:8; Za 34:19 Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena,
lakini waovu huangushwa chini na maafa.
17 #
Oba 1:12; Ay 31:29 Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo;
wakati ajikwaapo,
usiruhusu moyo wako ushangilie.
18 #
Ay 31:29
Bwana asije akaona na kuchukia
akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.
19 #
Za 37:1
Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya
wala usiwaonee wivu waovu,
20 #
Ay 18:5; Mit 13:9; Isa 3:11 kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo,
nayo taa ya waovu itazimwa.
21 #
Rum 13:1-7; 1Pet 2:17 Mwanangu, mche Bwana na mfalme,
wala usijiunge na waasi,
22 #
Za 73:19
kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao,
naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?
Misemo Zaidi Ya Wenye Hekima
23 #
Kut 18:16; Law 19:15; 2Nya 19:7; Za 72:2; Yer 22:16; Yn 7:24 Hii pia ni misemo ya wenye hekima:
Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema:
24 #
Isa 5:23; Mit 17:15 Yeyote amwambiaye mwenye hatia,
“Wewe huna hatia,”
Kabila zitamlaani
na mataifa yatamkana.
25Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia,
nazo baraka tele zitawajilia juu yao.
26Jawabu la uaminifu
ni kama busu la midomoni.
27 #
1Fal 5:17, 18; Lk 14:28 Maliza kazi zako za nje,
nawe uweke mashamba yako tayari,
baada ya hayo, jenga nyumba yako.
28 #
Za 7:4; Efe 4:25 Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu,
au kutumia midomo yako kudanganya.
29 #
Mit 20:22; Rum 12:17; Mt 5:39 Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi;
nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”
30 #
Mit 6:6-11; 26:13-16 Nilipita karibu na shamba la mvivu,
karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,
31 #
Yer 4:3; Ebr 6:8 miiba ilikuwa imeota kila mahali,
ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na
ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.
32Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona,
nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:
33 #
Mit 6:10
Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
34 #
Mit 10:4; Mhu 10:18 hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyang’anyi,
na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.