Mithali 26
NMM

Mithali 26

26
1 # Isa 32:6; 1Sam 12:17; Mit 19:10 Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno,
ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.
2 # Hes 23:8; Kum 23:5 Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake
au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi,
ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu.
3 # Za 32:9; Mit 10:13 Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,
nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu!
4 # Isa 36:21 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake,
ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.
5 # Mt 16:14; 21:24-27; Mit 3:7 Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake,
ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.
6 # Mit 10:26 Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara,
ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu.
7 # Mit 26:9 Kama miguu ya kiwete inavyoning’inia
ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu.
8 # Mit 26:1 Kama kufunga jiwe kwenye kombeo,
ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima.
9 # Mit 26:7 Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi
ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu.
10Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo,
ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani.
11 # Kut 8:15; Za 85:8; 2Pet 2:22 Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake,
ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake.
12 # Ufu 3:17; Mit 29:20 Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima
machoni pake mwenyewe?
Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
13 # Mit 6:6-11; 24:30-34; 22:13 Mvivu husema, “Yuko simba barabarani,
simba mkali anazunguka mitaa!”
14 # Mit 6:9 Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake,
ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.
15 # Mit 19:24 Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,
naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake.
16Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe,
kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
17Kama yeye amkamataye kwa mbwa masikio,
ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu.
18Kama mtu mwendawazimu
atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha,
19 # Efe 5:4 ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema,
“Nilikuwa nikifanya mzaha tu!”
20 # Mit 22:10 Bila kuni moto huzimika;
pasipo uchongezi ugomvi humalizika.
21 # Mit 14:17 Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto,
ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.
22 # Mit 18:8; Eze 22:9 Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;
huingia sehemu za ndani sana za mtu.
23 # Lk 22:48 Kama rangi ing’aayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo
ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya.
24 # Za 31:18; 41:6; Mit 10:18; Za 31:18; 41:6 Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake,
lakini moyoni mwake huficha udanganyifu.
25 # Za 28:3; Yer 9:4-8 Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini,
kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake.
26Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu,
lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.
27 # Za 7:15-16; 35:8; Mhu 10:8; Mit 28:10; Es 6:13; 7:9 Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake,
kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.
28 # Mit 13:6; 29:5; Za 12:3 Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza,
nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu