29
1 #
2Nya 36:16; Mit 6:15 Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi,
ataangamia ghafula, wala hapati dawa.
2 #
2Fal 11:20; Es 8:15; Mit 28:12 Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi;
waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.
3 #
1Fal 1:48; Mit 10:1; 23:15-16; 5:8-10; Lk 15:11-32 Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake,
bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.
4 #
Mit 8:15-16
Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti,
bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
5 #
Ay 32:21; Mit 26:28 Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili,
anautandaza wavu kuitega miguu yake.
6 #
Ay 5:13; Mhu 9:12 Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe
bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi.
7 #
Ay 29:16; Za 41:1; Isa 35:3-4 Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini,
bali mwovu hajishughulishi na hilo.
8 #
Mit 11:11; 16:14 Wenye mzaha huuchochea mji,
bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.
9 #
Mt 11:17
Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu,
mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
10 #
Mwa 4:5-8; 1Yn 3:12 Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu
na hutafuta kumuua mtu mnyofu.
11 #
Ay 15:13; Mit 12:16 Mpumbavu huonyesha hasira yake yote,
bali mwenye hekima hujizuia.
12 #
2Fal 21:9; Ay 34:30 Kama mtawala akisikiliza uongo,
maafisa wake wote huwa waovu.
13 #
Mit 22:2; Mt 5:45 Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili:
Bwana hutia nuru macho yao wote wawili.
14 #
Mit 29:4; Za 72:1-5; Mit 16:12 Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki,
kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.
15 #
Mit 29:17; 13:24 Fimbo ya maonyo hutia hekima,
bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo
humwaibisha mama yake.
16 #
Za 37:36; 58:10; 91:8 Wakati waovu wanapostawi,
pia dhambi vivyo hivyo,
lakini wenye haki wataliona anguko lao.
17 #
Mit 13:24; 29:15 Mrudi mwanao, naye atakupa amani,
atakufurahisha nafsi yako.
18 #
Za 19:11; Yn 13:17; Amo 8:11-12; 1Sam 3:1 Mahali pasipo na ufunuo, watu kujizuia,
bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
19Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu,
ajapoelewa, hataitikia.
20 #
Mit 14:17
Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka?
Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.
21Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani,
atamletea sikitiko mwishoni.
22 #
Mit 14:17
Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi,
naye mtu mwenye hasira ya haraka
hutenda dhambi nyingi.
23 #
Isa 66:2; Mt 23:12; Yak 4:6 Kiburi cha mtu humshusha,
bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu
hupata heshima.
24 #
Law 5:1
Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe;
huapishwa lakini hathubutu kushuhudia.
25 #
1Sam 15:24; Mit 28:25; 16:20 Kuwaogopa watu huwa ni mtego,
bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama.
26 #
Mit 19:6; 16:33 Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala,
bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana.
27 #
Mit 29:10
Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu;
waovu huwachukia sana wenye haki.