Zaburi 3
NMM

Zaburi 3

3
Zaburi 3
Sala Ya Asubuhi Ya Kuomba Msaada
Zaburi Ya Daudi Alipomkimbia Mwanawe Absalomu.
1 # 1Sam 15:12 Ee Bwana, tazama adui zangu walivyo wengi!
Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!
2 # Za 22:8; 22:7, 8; 71:11 Wengi wanasema juu yangu,
“Mungu hatamwokoa.”
3 # Mwa 15:1; Za 27:6; 2Fal 25:27 Lakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.
4 # Ay 30:20; Za 2:6; 27:6 Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu,
naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.
5 # Law 26:6; Mdo 12:6; Za 4:8; 17:15; 139:18; Mit 3:24 Ninajilaza na kupata usingizi;
naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.
6 # Za 23:4; 27:3; 118:11; Ay 11:15 Sitaogopa makumi elfu ya adui,
wanaojipanga dhidi yangu kila upande.
7 # 2Nya 6:41; Mt 6:13; Za 6:4; 7:1; 59:1; 57:4; 109:21; 119:153; Isa 25:9; 33:22; 35:4; 36:15; 37:20; Yer 42:11; Mao 3:16; Ay 16:10; 29:17; Mit 30:14 Ee Bwana, amka!
Niokoe, Ee Mungu wangu!
Wapige adui zangu wote kwenye taya,
vunja meno ya waovu.
8 # Za 27:1; 37:39; 62:1; Hes 6:23; Isa 43:3, 11; 44:6, 8; 45:21; Hos 13:4; Yon 2:9; Mit 21:31; Za 29:11; 129:8 Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana.
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu