4
Zaburi 4
Sala Ya Jioni Ya Kuomba Msaada
(Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Muziki. Zaburi Ya Daudi)
1 #
Za 13:3; 27:7; 69:16; 30:10; 54:2; 84:8; 88:2; 6:7; 102:2; Mwa 32:7; Amu 2:15 Nijibu nikuitapo,
Ee Mungu wangu mwenye haki!
Nipumzishe katika shida zangu;
nirehemu, usikie ombi langu.
2 #
Kut 16:7; Amo 2:4; 2Fal 19:26; Ay 8:22; Yer 13:25; 16:19; Za 12:1; 40:4; 1Sam 4:21 Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu
kuwa aibu mpaka lini?
Mtapenda udanganyifu
na kufuata miungu ya uongo mpaka lini?
3 #
Za 6:8; 12:1; 30:4; 31:23; 79:2; Mik 7:2, 7; Kut 33:16; 1Tim 4:7; 2Pet 3:11 Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga
wale wamchao kwa ajili yake;
Bwana atanisikia nimwitapo.
4 #
Efe 4:26; Za 63:6; Dan 2:28; Mit 3:7 #
Za 11:1; 25:20; 31:2; 32:11 Katika hasira yako, usitende dhambi.
Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya
mkiichunguza mioyo yenu.
5 #
Za 31:6; 37:3; 115:9; Mit 3:5; 28:26; Kum 33:19; Yn 14:1; Isa 26:4 #
Hes 14:18; Isa 65:6-7; Yer 32:17 Toeni dhabihu zilizo haki;
mtegemeeni Bwana.
6 #
Hes 6:25; Za 80:3 Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye
kutuonyesha jema lolote?”
Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako.
7 #
Mdo 14:17; Isa 9:3; 35:10; 65:14, 18; Mwa 27:28; Kum 28:51 Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa
kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.
8 #
Law 26:6; Hes 6:26; Yer 32:37; Ay 11:18; Flp 4:7; Kum 12:10; 33:28; Yn 14:27 #
Law 11:44
Nitajilaza chini na kulala kwa amani,
kwa kuwa wewe peke yako, Ee Bwana,
waniwezesha kukaa kwa salama.