5
Zaburi 5
Sala Kwa Ajili Ya Ulinzi Wakati Wa Hatari
(Kwa Mwimbishaji: Kwa Filimbi. Zaburi Ya Daudi)
1 #
1Fal 8:29; Za 17:1; 38:9; 40:1; 116:2; Dan 9:18; Isa 35:10; 51:11 Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu,
uangalie kupiga kite kwangu.
2 #
Ay 19:7; 24:12; 36:5; Za 44:4; 68:24; 84:3 Sikiliza kilio changu ili unisaidie,
Mfalme wangu na Mungu wangu,
kwa maana kwako ninaomba.
3 #
Isa 28:19; 50:4; Yer 21:12; Sef 3:5; Eze 46:13; Hab 2:1; Rum 8:19; Za 30:5; 62:1; 119:81; 130:5 Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana;
asubuhi naleta haja zangu mbele zako,
na kusubiri kwa matumaini.
4 #
Za 1:5; 11:5; 104:35; Mit 2:22; Mal 2:17 Wewe si Mungu unayefurahia uovu,
kwako mtu mwovu hataishi.
5 #
2Fal 19:32; Za 1:5; 45:10; 1:3; 119:104; 73:3; 75:4; 14:1; Isa 33:19; 37:33; Mit 8:13; Hab 1:13 Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako,
unawachukia wote watendao mabaya.
6 #
Mit 19:22; Yn 8:44; Mdo 5:3; Ufu 21:8 Unawaangamiza wasemao uongo.
Bwana huwachukia
wamwagao damu na wadanganyifu.
7 #
Kum 13:4; Yer 44:10; Dan 6:26; 2Sam 12:16; Za 138:2; 1Fal 8:48 Lakini mimi, kwa rehema zako kuu,
nitakuja katika nyumba yako,
kwa unyenyekevu, nitasujudu
kuelekea Hekalu lako takatifu.
8 #
Za 23:3; 31:1; 71:2; 85:13; 89:16; Mit 8:20; 1Fal 8:36; Yn 1:23 Niongoze katika haki yako, Ee Bwana,
kwa sababu ya adui zangu,
nyoosha njia yako mbele yangu.
9 #
Yer 5:16; Lk 11:44; Za 12:2; 28:3; 36:3; Yer 9:8; Rum 3:13 #
Isa 13:8; Yer 46:5 Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika,
mioyo yao imejaa maangamizi.
Koo lao ni kaburi lililo wazi,
kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu.
10 #
Mao 1:5; 3:42; Za 78:40; 106:7; 107:11 Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu!
Hila zao ziwe anguko lao wenyewe.
Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi,
kwa kuwa wamekuasi wewe.
11 #
1Kor 2:9; Za 33:1; 81:1; 90:14; 92:4; 95:1; 145:7; 69:36; 119:132; Ay 22:19 Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi,
waimbe kwa shangwe daima.
Ueneze ulinzi wako juu yao,
ili wale wapendao jina lako
wapate kukushangilia.
12 #
Za 112:2; 32:7; Mwa 15:1 Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki,
unawazunguka kwa wema wako kama ngao.