Zaburi 7
NMM

Zaburi 7

7
Zaburi 7
Sala Ya Mtu Anayedhulumiwa
(Ombolezo La Daudi Kwa Bwana Kwa Sababu Ya Kushi, Mbenyamini)
1 # Za 2:12; 11:1; 31:1; 3:7; 31:15; 119:86, 157, 161 Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe,
uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia,
2 # Mwa 49:9; Ufu 4:7; Za 3:2; 71:11; 1Pet 5:8 la sivyo watanirarua kama simba
na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa.
3 # Za 35:7, 19; Mit 24:28; 1Sam 24:7 Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya
na kuna hatia mikononi mwangu,
4 # Za 35:7, 19; Mit 24:28; 1Sam 24:7 au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami,
au nimemnyang’anya adui yangu pasipo sababu,
5 # Kut 15:9; Ay 7:21; 2Sam 22:43; 2Fal 9:33; Isa 10:6; Mao 3:16 basi adui anifuatie na kunipata,
auponde uhai wangu ardhini
na kunilaza mavumbini.
6 # 2Nya 6:41; Za 138:7; 35:23; 44:23; 94:2 Amka kwa hasira yako, Ee Bwana,
inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu.
Amka, Mungu wangu, uamue haki.
7 # Za 68:18 Kusanyiko la watu na likuzunguke.
Watawale kutoka juu.
8 # 1Nya 16:33; Mk 5:7; 1Sam 26:23; Za 18:20; Mwa 3:5; 20:5; Hes 24:16 Bwana na awahukumu kabila za watu.
Nihukumu Ee Bwana,
kwa kadiri ya haki yangu,
kwa kadiri ya uadilifu wangu,
Ewe Uliye Juu Sana.
9 # Yer 11:20; Ufu 2:23; Za 26:2; 37:23; 40:2; 1Sam 16:7; 1Nya 28:9 Ee Mungu mwenye haki,
uchunguzaye mawazo na mioyo,
komesha ghasia za waovu
na ufanye wenye haki waishi kwa amani.
10 # Za 3:3; Ay 33:3 Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana,
awaokoaye wanyofu wa moyo.
11 # Mwa 18:25; Za 9:8; 67:4; 75:2; 96:13; 98:9; Isa 11:4; Yer 11:20 Mungu ni mwamuzi mwenye haki,
Mungu aghadhibikaye kila siku.
12 # Eze 3:19; 33:9; Kum 32:4; Za 21:12; 2Sam 22:35; Isa 5:28; 13:18 Kama hakutuhurumia,
atanoa upanga wake,
ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.
13 # Za 11:2; 18:14; 64:3 Ameandaa silaha zake kali,
ameweka tayari mishale yake ya moto.
14 # Isa 59:4; Yak 1:15 Yeye aliye na mimba ya uovu
na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.
15 # Za 35:7, 8; 40:2; 94:13; Mit 26:27; Ay 4:8; Es 7:10; Mit 5:22 Yeye achimbaye shimo na kulifukua
hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.
16 # 1Fal 2:23 Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe,
ukatili wake humrudia kichwani.
17 # 2Nya 31:2; Za 5:8; Rum 15:11; Mwa 14:18; Ebr 2:12 Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake,
na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu