Zaburi 8
NMM

Zaburi 8

8
Zaburi 8
Utukufu Wa Mungu Na Heshima Ya Mwanadamu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Daudi)
1 # 1Nya 16:10; Lk 2:9; Hab 3:3; Kut 15:11; Za 57:5; 108:5; 113:4; 148:13 Ee Bwana, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Umeuweka utukufu wako
juu ya mbingu.
2 # Mt 11:25; 21:16; Za 143:12; 1Kor 1:27 Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao
umeamuru sifa,
kwa sababu ya watesi wako,
kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi.
3 # Mwa 1:16; 15:5; Kum 10:14; Kut 8:19; 1Kor 15:41; 1Nya 16:26; 2Nya 2:12; Za 102:25 Nikiziangalia mbingu zako,
kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota,
ulizoziratibisha,
4 # 1Nya 29:14; Ebr 2:6; Ay 7:17; Za 144:3 mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria,
binadamu ni nani hata unamjali?
5 # Mwa 1:26; Za 21:5; 103:4 Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni,
ukamvika taji ya utukufu na heshima.
6 # Mwa 1:28; Ay 10:3; Za 19:1; 102:25; 145:10; Isa 26:12; 29:23; 45:11; Ebr 1:10; 2:6-8; 1Fal 5:3; 1Kor 15:25, 27; Efe 1:22; 1Kor 15:27 Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako;
umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.
7 # Mwa 13:5; 26:14; 2:19 Mifugo na makundi yote pia,
naam, na wanyama wa kondeni,
8 # Mwa 1:26 ndege wa angani na samaki wa baharini,
naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari.
9 # Ay 11:7; Za 35:10 Ee Bwana, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu