16
Mabakuli Saba Ya Ghadhabu Ya Mungu
1 #
Ufu 15:1; Ufu 11:19; 15:1; 16:2-21; Za 79:6; Sef 3:8 Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mle Hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, “Nendeni, mkayamwage duniani hayo mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.”
2 #
Ufu 8:7; 13:15; 17; Kut 9:9-11 Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.
3 #
Kut 7:17-21; Ufu 6:11 Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
4 #
Ufu 8:10
Malaika wa tatu akalimwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikawa damu. 5#Ufu 15:3-4; Ufu 15:3; 1:4; 15:4; 6:10Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema:
“Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa,
wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu,
kwa sababu umehukumu hivyo;
6 #
Isa 49:26
kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako
na manabii wako,
nawe umewapa damu wanywe
kama walivyostahili.”
7 #
Ufu 9:6; 15:3; 19:2 Nikasikia madhabahu ikiitikia,
“Naam, Bwana Mwenyezi Mungu,
hukumu zako ni kweli na haki.”
8 #
Ufu 8:12; 14:18 Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua, nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto. 9#Ufu 2:21; 11:13Watu wakaunguzwa na hilo joto kali, wakalaani Jina la Mungu, aliyekuwa na uwezo juu ya mapigo haya, tena wakakataa kutubu na kumtukuza Mungu.
10 #
Ufu 13:2; 9:2 Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha enzi cha yule mnyama, nao ufalme wake ukagubikwa na giza. Watu wakatafuna ndimi zao kwa ajili ya maumivu, 11#Ufu 11:13; 2:21; Ufu 16:9, 21wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu na majeraha yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.
12 #
Ufu 9:14; Isa 41:2 Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa Frati, maji yake yakakauka ili kutayarisha njia kwa ajili ya wafalme watokao Mashariki. 13#Ufu 12:3; 13:1; Ufu 19:20Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14#1Tim 4:1; Ufu 17:14Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mwenyezi Mungu.
15 #
Lk 12:3
“Tazama, naja kama mwizi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuonekana aibu yake.”
16 #
Ufu 9:11; Amu 5:19 Ndipo wakawakusanya wafalme pamoja mahali paitwapo Armagedoni#16:16 Armagedoni au Har-Magedoni ina maana Mlima Megido, mahali pa kinabii ambapo wafalme wote wa dunia watakusanyika kwa vita katika siku ya Mwenyezi Mungu. kwa Kiebrania.
17 #
Efe 2:2; Ufu 14:15; 11:15; Ufu 21:6 Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!” 18#Ufu 4:5; 6:12; Dan 12:1Kukawa na mianga ya umeme wa radi, ngurumo, radi na tetemeko kubwa la ardhi. Hapajawa kamwe na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, hivyo lilikuwa tetemeko kubwa ajabu. 19#Ufu 17:18; 18:5; Ufu 14:8Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu akaukumbuka Babeli Mkuu na kumpa kikombe kilichojaa mvinyo wa ghadhabu ya hasira yake. 20#Ufu 6:14Kila kisiwa kikatoweka wala milima haikuonekana. 21#Eze 13:13; Kut 9:23-25Mvua kubwa ya mawe yenye uzito wa talanta moja#16:21 Talanta moja ni kama kilo 34. ikashuka kutoka mbinguni, ikawaangukia wanadamu. Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha.