Warumi 9
NMM

Warumi 9

9
Kuteuliwa Kwa Israeli Na Mungu
1 # Gal 1:20; 1Tim 2:7; Rum 1:9 Ninasema kweli katika Al-Masihi, wala sisemi uongo, dhamiri yangu inanishuhudia katika Roho Mtakatifu. 2#Rum 10:1Nina huzuni kuu na uchungu usiokoma moyoni mwangu. 3#Kut 32:32; 1Kor 12:3; 16:22; Rum 11:14Kwa maana ningetamani hata mimi nilaaniwe na kutengwa na Al-Masihi kwa ajili ya ndugu zangu hasa, wale walio wa kabila langu kwa jinsi ya mwili, 4#Kut 6:7; Kum 7:6; 4:13; Flp 1:12; Za 147:19; Ebr 9:1; Mdo 13:32; Gal 3:16yaani, watu wa Israeli, ambao ndio wenye kule kufanywa wana, ule utukufu wa Mungu, yale maagano, kule kupokea sheria, ibada ya kwenye Hekalu na zile ahadi. 5#Mt 1:1-16; Yn 1:1; Kol 2:9; Rum 1:3, 25; 2Kor 11:31Wao ni wa uzao wa mababa wakuu wa kwanza, ambao kutoka kwao Al-Masihi alikuja kwa jinsi ya mwili kama mwanadamu, yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, mwenye kuhimidiwa milele! Amen.
6 # Rum 2:28, 29; Gal 6:16 Si kwamba Neno la Mungu limeshindwa. Kwa maana si kila Mwisraeli ambaye ni wa uzao utokanao na Israeli ni Mwisraeli halisi. 7#Mwa 21:12; Ebr 11:18Wala hawakuwi wazao wa Ibrahimu kwa sababu wao ni watoto wake, lakini: “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaka.” 8#Rum 8:14; Gal 3:16; 4:23Hii ina maana kwamba, si watoto waliozaliwa kimwili walio watoto wa Mungu, bali ni watoto wa ahadi wanaohesabiwa kuwa uzao wa Ibrahimu. 9#Mwa 18:10; Mwa 18:14Kwa maana ahadi yenyewe ilisema, “Nitakurudia tena wakati kama huu, naye Sara atapata mtoto wa kiume.”
10 # Mwa 25:23; Mwa 25:21 Wala si hivyo tu, bali pia watoto aliowazaa Rebeka walikuwa na baba huyo huyo mmoja, yaani, baba yetu Isaka. 11#Rum 8:28; Rum 9:16; 8:28Lakini, hata kabla hao mapacha hawajazaliwa au kufanya jambo lolote jema au baya, ili kwamba kusudi la Mungu la kuchagua lipate kusimama, 12#Mwa 25:23si kwa matendo, bali kwa yeye mwenye kuita, Rebeka aliambiwa, “Yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.” 13#Mal 1:2-3; Kum 21:15; Mit 13:24; Mt 10:37; Lk 14:26; Yn 12:25Kama vile ilivyoandikwa, “Nimempenda Yakobo, lakini nimemchukia Esau.”
Mungu Hana Upendeleo
14 # 2Nya 19:7; Kum 32:4; Ay 8:3; 34:10; Za 92:15 Tuseme nini basi? Je, Mungu ni dhalimu? La, hasha! 15#Kut 33:19Kwa maana Mungu alimwambia Musa,
“Nitamrehemu yeye nimrehemuye,
na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.”
16 # Efe 2:8; Tit 3:5 Kwa hiyo haitegemei kutaka kwa mwanadamu au jitihada, bali hutegemea huruma ya Mungu. 17#Kut 14:4; Za 76:10Kwa maana Maandiko yamwambia Farao, “Nilikuinua kwa kusudi hili hasa, ili nipate kuonyesha uweza wangu juu yako, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote.”
18 # Yos 11:20; Rum 11:25 Kwa hiyo basi, Mungu humhurumia yeye atakaye kumhurumia na humfanya mgumu yeye atakaye kumfanya mgumu.
19 # 1Kor 15:35; Yos 2:18; 2Sam 16:10; Dan 4:35 Basi mtaniambia, “Kama ni hivyo, kwa nini basi bado Mungu anatulaumu? Kwa maana ni nani awezaye kupinga mapenzi yake?” 20#Isa 64:8; Yer 18:6; Isa 10:15Lakini, ewe mwanadamu, u nani wewe ushindane na Mungu? “Je, kilichoumbwa chaweza kumwambia yeye aliyekiumba, ‘Kwa nini umeniumba hivi?’ ” 21#2Tim 2:20Je, mfinyanzi hana haki ya kufinyanga kutoka bonge moja vyombo vya udongo, vingine kwa matumizi ya heshima na vingine kwa matumizi ya kawaida?
22 # Rum 2:4 Iweje basi, kama Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na kufanya uweza wake ujulikane, amevumilia kwa uvumilivu mwingi vile vyombo vya ghadhabu vilivyoandaliwa kwa uharibifu? 23#Rum 8:28; 8:30Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vile vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake, 24#Rum 8:28; 3:29yaani pamoja na sisi, ambao pia alituita, si kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa?
Yote Yalitabiriwa Katika Maandiko
25 # Hos 2:23; 1Pet 2:10 Kama vile Mungu asemavyo katika Hosea:
“Nitawaita ‘watu wangu’
wale ambao si watu wangu;
nami nitamwita ‘mpenzi wangu’
yeye ambaye si mpenzi wangu,”
26 # Hos 1:10; Mt 16:16 tena,
“Itakuwa hasa mahali pale walipoambiwa,
‘Ninyi si watu wangu,’
wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ ”
27 # Mwa 22:17; Isa 10:22-23; Hos 1:10; Yoe 2:32; Rum 11:5 Isaya anapiga kelele kuhusu Israeli:
“Ingawa idadi ya wana wa Israeli
ni wengi kama mchanga wa pwani,
ni mabaki yao tu watakaookolewa.
28Kwa kuwa Bwana ataitekeleza
hukumu yake duniani kwa haraka
na kwa ukamilifu.”
29 # Yak 5:4; Isa 1:9; 13:19; Yer 50; 40 Ni kama vile alivyotabiri Isaya akisema:
“Kama Bwana Mwenye Nguvu Zote
asingelituachia uzao,
tungelikuwa kama Sodoma,
tungelifanana na Gomora.”
Kutokuamini Kwa Israeli
30 # Flp 3:9; Ebr 11:17 Kwa hiyo tuseme nini basi? Kwamba watu wa Mataifa ambao hawakutafuta haki, wamepata haki ile iliyo kwa njia ya imani. 31#Isa 51:11; Rum 11:7; Gal 5:4Lakini Israeli, ambao walijitahidi kupata haki kwa njia ya sheria, hawakuipata. 32#1Pet 2:8Kwa nini? Kwa sababu hawakuitafuta kwa njia ya imani bali kwa njia ya matendo. Wakajikwaa kwenye lile “jiwe la kukwaza.” 33#Isa 8:14; 1Pet 2:6, 8Kama ilivyoandikwa:
“Tazama naweka katika Sayuni jiwe la kukwaza watu
na mwamba wa kuwaangusha.
Yeyote atakayemwamini
hataaibika kamwe.”

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu