Ruthu Utangulizi
NMM

Ruthu Utangulizi

Utangulizi
Kitabu cha Ruthu kinaonyesha upande mwingine wa maisha wakati wa machafuko katika utawala wa waamuzi. Katika kitabu hiki kuna faraja au tulizo kutoka umwagaji wa damu na vurugu ambazo zilionekana kumeza nchi kwa sababu ya dhambi ya Israeli. Ni hadithi ya Ruthu, ambaye aliamua kukaa na mama mkwe wake Naomi baada ya msiba kumpata. Mwenyezi Mungu alimrudishia Ruthu wema kwa kumpa mume (yaani Boazi) na mtoto, na pia kwake Naomi kwa kumpa wajukuu. Kutoka familia hii mwishowe alitokea Mfalme Daudi.
Wazo Kuu
Kiini cha kitabu hiki ni kwamba hata wakati wa wasiwasi mwingi au migogoro na kukata tamaa, tunaweza kuishi maisha kulingana na mwongozo wa Mwenyezi Mungu. Pia Mwenyezi Mungu huwabariki zaidi wale ambao huishi vile. Maadili ya kimsingi ya binadamu ya upendo, imani, tumaini na wema ni makuu zaidi kuliko chuki na vurugu za binadamu, na huendelea kutoka vizazi hadi vingine kama mwanga wa kuongoza wale wanaotafuta maana ya kweli ya maisha.
Mwandishi
Hajulikani.
Tarehe
Wakati wa utawala wa Waamuzi.
Mgawanyo
• Msiba wa Naomi (1:1-10)
• Uaminifu wa Ruthu kwa Naomi (1:11-22)
• Urafiki wa Boazi (2:1–3:18)
• Ndoa ya Boazi na Ruthu (4:1-17)
• Ukoo wa Mfalme Daudi (4:18-22).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu