Wimbo 1
NMM

Wimbo 1

1
1 # 1Fal 4:32; Za 45 Wimbo ulio bora wa Sulemani.
Shairi La Kwanza
Mpendwa
2 # Wim 8:6; Mwa 14:18; Amu 9:13; Wim 4:10 Unibusu kwa busu la kinywa chako,
kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.
3 # Es 2:12; Za 45:8-14; Mhu 7:1 Manukato yako yananukia vizuri,
jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa.
Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!
4 # Yer 31:3; Flp 3:12; Wim 2:3 Nichukue twende nawe, na tufanye haraka!
Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake.
Marafiki
Tunakushangilia na kukufurahia,
tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai.
Mpendwa
Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!
5 # Wim 2:14; 2:7; 5:16; 4:3; Mwa 25:13 Mimi ni mweusi, lakini napendeza,
enyi binti za Yerusalemu,
mweusi kama mahema ya Kedari,
kama mapazia ya hema la Sulemani.
6 # Za 69:8; Wim 7:12; 8:12; 2:15 Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi,
kwa sababu nimefanywa mweusi na jua.
Wana wa mama yangu walinikasirikia
na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu.
Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.
7 # Wim 3:1-4; Isa 13:20; Mwa 24:65 Niambie, wewe ambaye ninakupenda,
unalisha wapi kundi lako la kondoo
na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri.
Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela
karibu na makundi ya rafiki zako?
Marafiki
8 # Wim 5:9; 6:1 Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote,
fuata nyayo za kondoo,
na kulisha wana-mbuzi wako
karibu na hema za wachungaji.
Mpenzi
9 # Wim 2:2; 2Nya 1:16-17 Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike
aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.
10 # Eze 16:11; Isa 61:10; Wim 5:13 Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli,
shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.
11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu,
vyenye kupambwa kwa fedha.
Mpendwa
12 # Wim 4:11-14 Wakati mfalme alipokuwa mezani pake,
manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.
13 # Mwa 37:25 Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane
kati ya matiti yangu.
14 # Wim 4:13; 1Sam 23:29 # 2Nya 20:2; Wim 2:3; 5:8 Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina
kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi.
Mpenzi
15 # Wim 4:7; 7:6; Za 74:19; Yer 48:28 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
Tazama jinsi ulivyo mzuri!
Macho yako ni kama ya hua.
Mpendwa
16Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
Ee, tazama jinsi unavyopendeza!
Na kitanda chetu ni cha majani mazuri.
Mpenzi
17 # 1Fal 6:9 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi,
na mapao yetu ni miberoshi.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu