Wimbo Utangulizi
NMM

Wimbo Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kinahusu upendo wa Sulemani na mwanamke Mshulami. Kinajumuisha mfululizo wa mashairi au nyimbo, ndiyo maana kikaitwa: Wimbo ulio Bora. Ni kitabu rahisi lakini cha kusisimua, kikielezea mvuto wa wapenzi wawili mmoja kwa mwingine, shida ambazo zapaswa kutatuliwa, hisia tulivu za mapenzi ambazo upendo huibua, na furaha wanayopata wapenzi hawa wawili kwa kuwa pamoja. “Wanawake wa Yerusalemu,” wanaotokea na Sulemani na mpenzi wake, wanaongezea utamu wa hadithi hii kwa kuchangia maoni yao.
Wazo Kuu
Maana iliyo dhahiri ya wimbo huu ni kwamba mapenzi ya wanadamu, yaliyoanzishwa na Mwenyezi Mungu, ni mema na matakatifu yanapofurahiwa kwa kutii amri za Mungu. Wasomi wengi wameona maana ya kiashiria katika hadithi hii, hata hivyo, na wanafikiria yote inalenga upendo wa Mungu kwa Israeli, au upendo wa Al-Masihi kwa kanisa lake. Mtazamo huu unakazia mafunzo ya Injili kwamba Mungu ni upendo (1 Yohana 4:8).
Mwandishi
Sulemani.
Tarehe
Karne ya 10 K.K.
Mgawanyo
• Shauku ya mwanamwali Mshulami kwa Sulemani (1:1–2:17)
• Mwanamwali Mshulami na wanawake wa Yerusalemu (3:1-11)
• Kuingia rasmi kwa Sulemani (4:1–6:13)
• Sulemani akiwa pekee na mpenzi wake (7:1–8:14).

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu