Utangulizi
Zekaria alikuwa mwenza wa Hagai na alitumwa na Mwenyezi Mungu kwa jamii iliyokuwa imerejeshwa kuwatia moyo watu ili kumtumikia Mwenyezi Mungu bila uoga. Kitabu kinaanza kwa mfululizo wa maono nane ambayo yanaonyesha kwa lugha ya ishara na picha uwezo wa Mwenyezi Mungu, na pia mamlaka ya Mwenyezi Mungu juu ya mambo ya binadamu, umuhimu wa nguvu za kiroho, hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa dhambi, na ahadi ya mambo yatakayokuja. Sehemu muhimu zaidi katika nakala hii ni unabii kuhusu kuja kwa Al-Masihi.
Wazo Kuu
Riziki ya Mwenyezi Mungu, aliye Bwana juu ya vyote, kwa mahitaji ya watu wake ndicho kiini cha kitabu hiki. Mwenyezi Mungu huwapa watu wake ulinzi, ufanisi, nguvu na neema. Hitaji lao kubwa zaidi ni kumjua Mwenyezi Mungu vyema, nalo hili atalikidhi kwa kumtuma Masiya, aliye Bwana Isa Al-Masihi.
Mwandishi
Zekaria.
Tarehe
Kuanzia 520 K.K.
Mgawanyo
• Utangulizi (1:1-6)
• Maono nane ya kinabii (1:7–6:8)
• Kutawazwa kwa Yoshua kinabii (6:9-15)
• Jumbe mbali mbali za hukumu na matumaini (7:1–10:12)
• Kuja kwa Masiya na kukataliwa kwake (11:1–13:9)
• Ushindi mwishowe wa Masiya (14:1-21).