Sefania 2
NMM

Sefania 2

2
1 # 2Nya 20:4; Yoe 1:14; 2:16; Yer 3:3; 6:15 Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja,
enyi taifa lisilo na aibu,
2 # Isa 17:13; Hos 13:3; 2Fal 23:26; Yer 4:4; 10:25; Eze 7:19; Mao 4:11 kabla ya wakati ulioamriwa haujafika
na siku ile inayopeperusha kama makapi,
kabla hasira kali ya Bwana haijaja juu yenu,
kabla siku ya ghadhabu ya Bwana
haijaja juu yenu.
3 # Amo 5:6; Yoe 2:4; Isa 1:17; Za 45:4; 57:1; 76:9 Mtafuteni Bwana, enyi nyote wanyenyekevu wa nchi,
ninyi ambao hufanya lile analoamuru.
Tafuteni haki, tafuteni unyenyekevu;
labda mtahifadhiwa
siku ya hasira ya Bwana.
Dhidi Ya Ufilisti
4 # Mwa 10:19; Amo 1:6-8; Zek 9:5-7; Yer 6:4; 47:5 Gaza utaachwa
na Ashkeloni utaachwa magofu.
Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupu
na Ekroni utang’olewa.
5 # 1Sam 30:14; Law 26:31; Eze 25:16; Yos 13:3; Isa 14:30 Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari,
enyi Wakerethi;
neno la Bwana liko dhidi yenu,
ee Kanaani, nchi ya Wafilisti.
“Mimi nitawaangamiza,
na hakuna atakayebaki.”
6 # Isa 5:17; 17:2 Nchi kando ya bahari, mahali ambapo wanaishi Wakerethi,
patakuwa mahali pa wachungaji
na mazizi ya kondoo.
7 # Isa 11:11; Hag 1:12; Mik 5:7; 4:10; Kut 4:31; Lk 1:68; Mwa 45:7; Kum 30:3; Za 126:4; Yer 23:3; 32:44; Hos 6:11; Eze 39:25; Yoe 3:1; Amo 1:6-8 Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda,
hapo watapata malisho.
Wakati wa jioni watajilaza chini
katika nyumba za Ashkeloni.
Bwana Mwenyezi Mungu wao atawatunza,
naye atawarudishia wafungwa wao.
Dhidi Ya Moabu Na Amoni
8 # Mwa 19:37; Yer 48:27; 49:1; Eze 25:3, 8; 21:28; Mao 3:61; Isa 16:6 “Nimeyasikia matukano ya Moabu
nazo dhihaka za Waamoni,
ambao waliwatukana watu wangu
na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao.
9 # Kum 23:6; 29:23; Isa 11:14; Yer 48:1-47; 49:1-6; Eze 25:1-11; 2Fal 19:31; Amo 1:13; 2:1-3 Hakika, kama niishivyo,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mungu wa Israeli,
“hakika Moabu itakuwa kama Sodoma,
Waamoni kama Gomora:
mahali pa magugu na mashimo ya chumvi,
nchi ya ukiwa milele.
Mabaki ya watu wangu watawateka nyara;
mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”
10 # Ay 40:12; Isa 16:6; Yer 48:27; Za 9:6 Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao,
kwa kutukana na kudhihaki
watu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote.
11 # Mwa 49:10; 10:5; Za 2:8; 22:27; Isa 2:2, 3; Mal 1:11; Yn 4:21; 1Tim 2:8; Yoe 2:11; 1Nya 19:1; Eze 25:6-7; Isa 12:4; Za 86:9; Sef 3:9 Bwana atakuwa wa kuhofisha kwao
atakapoangamiza miungu yote ya nchi.
Mataifa katika kila pwani yatamwabudu,
kila moja katika nchi yake.
Dhidi Ya Kushi
12 # Mwa 10:6; Isa 18:1; 20:4; Yer 46:10 “Ninyi pia, ee Wakushi,
mtauawa kwa upanga wangu.”
Dhidi Ya Ashuru
13 # Mwa 10:5-11; Zek 10:11; Mik 5:6 Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazini
na kuangamiza Waashuru,
akiiacha Ninawi ukiwa
na pakame kama jangwa.
14 # Isa 5:17; 13:21; 14:23; Ufu 18:2; Za 102:6 Makundi ya kondoo na ng’ombe yatajilaza pale,
viumbe vya kila aina.
Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba
wataishi juu ya nguzo zake.
Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani,
kifusi kitakuwa milangoni,
boriti za mierezi zitaachwa wazi.
15 # Isa 32:9; 47:8; Eze 27:36; 28:2; Ufu 18:7; Yer 49:33; Nah 3:19 Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furaha
wakijisikia salama.
Ulisema moyoni mwako,
“Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila mimi.”
Jinsi gani umekuwa gofu,
mahali pa kulala wanyama pori!
Wote wanaopita kando yake wanauzomea
na kutikisa mkono kwa dharau.

Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu)

Copyright © 2018 by Biblica, Inc.®

All Rights Reserved Worldwide.

Learn More About Neno: Maandiko Matakatifu