Utangulizi
Sefania alikuwa nabii kwa Yuda katika siku za mwisho za kuwepo kwa Yuda kabla haijaharibiwa mnamo 586 KK. Yosia ndiye alikuwa mfalme wakati Sefania alikuwa akihubiri. Alichangamshwa kiasi na ujumbe wa Sefania, hivyo akaanzisha mabadiliko katika mwaka wa 621 KK. Lakini mabadiliko haya, kusema ukweli, yalikuwa madogo sana na yamechelewa. Watu walirudi katika njia zao za uovu, na mji kuanguka kwa wavamizi kutoka Babeli. Ujumbe wa Sefania ni ujumbe mkali, uliojengwa katika msingi wa hukumu ya haki ya Mwenyezi Mungu. Sio Yuda pekee watauhisi mkono mzito wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya dhambi zao, bali pia mataifa yote jirani.
Wazo Kuu
Watu wa Yuda walitumaini kwamba licha ya dhambi zao, wakati wa siku ya Bwana (yaani siku ya hukumu) ukiwadia, Mwenyezi Mungu angewapendelea lakini awe mkali kwa maadui zao. Sefania anawaambia ya kwamba Mwenyezi Mungu anapohukumu dhambi, wale ambao wanajua mengi zaidi ndio wanahangaika zaidi. Hukumu itaanza na Yuda na kumalizia na mataifa mengine. Lakini ikiwa Yuda itatubu kutoka moyoni, basi Mwenyezi Mungu atageuza hukumu yake na kuwapa uhai na baraka.
Mwandishi
Sefania.
Tarehe
Kabla ya 621 K.K.
Mgawanyo
• Kutangaza hukumu inayokuja ya Mwenyezi Mungu (1:1–2:3)
• Hukumu dhidi ya mataifa na Yerusalemu (2:4–3:8)
• Yuda kuahidiwa baraka (3:9-20).