Yuda UTANGULIZI
SCLDC10

Yuda UTANGULIZI

UTANGULIZI
Barua hii ya Yuda imeandikwa sio kwa jumuiya fulani ya kanisa, bali kwa jumuiya yote ya Kikristo. Mwandishi anajitaja kama “Yuda, nduguye Yakobo”. Katika Injili ya Marko hao wawili, Yuda na Yakobo, wanasemekana kuwa “nduguze Yesu”. Tunajua mengi juu ya Yakobo, kwamba yeye alikuwa na nafasi muhimu ya uongozi wa jumuiya ya waumini wa Kanisa la Yerusalemu, na pia mwandishi wa barua inayotajwa kwa jina lake. Lakini hatujui mengine juu ya Yuda.
Mwandishi anatuambia kwamba alikuwa na lengo lake la kuandika juu ya msingi wa imani, lakini akalazimika kubadili na kuandika barua hii ya kuwashutumu waenezi wa mafundisho ya uongo ambao walijipenyeza kwa siri katika jumuiya ya waumini (3-16). Mwandishi anawaonya waumini wadumu imara katika imani (17-23) na kumalizia kwa utenzi wa sifa “kwake yeye aliye peke yake Mungu, Mkombozi wetu, uwe utukufu, ukuu, nguvu na mamlaka kwa njia ya Kristo Bwana wetu, tangu zama zote, sasa na hata milele! Amina” (24-25).

Swahili Common Language DC Bible: Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki © Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya, 1995, 2001. Haki zote zimehifadhiwa.  

Learn More About BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA