Sira UTANGULIZI
SCLDC10

Sira UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu cha Hekima ya Sira (chajulikana pia kama “Eklesiastiko”) hapo awali kilikuwa kimeandikwa kwa Kiebrania yapata mwaka 180 K.K. Kitabu hiki kilitafsiriwa kwa Kigiriki na mjukuu wake. Mwandishi anatia sahihi kitabu chake kwa jina (50:27) na kusema juu ya kazi yake (39:1-11). Tunaambiwa hivyo na huyo mwana mjukuu katika utangulizi wa kitabu hiki. Makala ya Kigiriki ndiyo iliyotumiwa kutoa tafsiri hii ya Kiswahili.
Kitabu chenyewe ni kimojawapo cha vitabu vijulikanavyo kama vitabu vya hekima, nacho chajumuika na umoja wa vitabu hivyo vya Agano la Kale katika kuonesha umoja wa maandishi ya sheria, maandishi ya manabii na ya vitabu vingine; hili ni jambo linalosisitizwa katika kitabu hiki, pamoja na mafunzo kuhusu uzoefu na “kumcha Bwana.” Ingawa Sira hakina muundo dhahiri, kinafanana na kitabu cha Methali kwa namna nyingi. Kinasisitiza mafundisho yaliyo kawaida ya hekima: Usemi unaofaa, utajiri na umaskini, uaminifu, nidhamu, uchaguzi wa marafiki, dhambi na kifo, tuzo na hekima.

Swahili Common Language DC Bible: Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki © Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya, 1995, 2001. Haki zote zimehifadhiwa.  

Learn More About BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA