2 Mambo ya Nyakati 14
RSUVDC

2 Mambo ya Nyakati 14

14
Asa atawala
1 # 1 Fal 15:8 Basi Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi, akatawala Asa mwanawe mahali pake; katika siku zake nchi ikastarehe miaka kumi.
2Basi, Asa akafanya yaliyo mema, yaliyo ya adili, machoni pa BWANA, Mungu wake; 3#1 Fal 15:14; 2 Nya 15:17; Kut 34:13; 1 Fal 11:7 maana aliziondoa madhabahu za kigeni, na mahali pa juu, akazivunja nguzo, akayakatakata maashera; 4akawaamuru Yuda wamtafute BWANA, Mungu wa baba zao, na kuzitenda torati na amri. 5Tena akaondoa kutoka miji yote ya Yuda mahali pa juu na sanamu za jua; ufalme ukastarehe mbele yake. 6Akajenga miji yenye maboma katika Yuda; kwa kuwa nchi ilikuwa imestarehe, wala hakuwa na vita miaka ile; kwa sababu BWANA alimpa amani. 7Naye akawaambia Yuda, Na tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo; nchi bado ingali ipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta BWANA, Mungu wetu; naam, tumemtafuta, naye ametustarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa. 8Naye Asa alikuwa na jeshi waliochukua ngao na mikuki, katika Yuda elfu mia tatu; na katika Benyamini wenye kuchukua vigao na kupinda upinde, elfu mia mbili na themanini; hao wote walikuwa mashujaa.
Uvamizi wa Kushi wazimwa
9 # 2 Nya 16:8; Yos 15:44; Mik 1:15 Kisha, Zera Mkushi alikuja kuwashambulia akiwa na jeshi la watu milioni moja na magari mia tatu akaja Maresha. 10Asa akatoka kukutana naye, wakapanga vita Maresha bondeni mwa Sefatha. 11#Kut 14:10; 1 Nya 5:20; 2 Nya 13:14; Zab 22:5; Mdo 2:21; Amu 7:7; 1 Sam 14:6; 2 Kor 12:9,10; 1 Sam 17:45; Mit 18:10; Nah 1:7 Naye Asa akamlilia BWANA, Mungu wake, akasema, BWANA, hapana kuliko wewe aliye wa kusaidia, kati yake yeye aliye hodari, na yeye asiye na nguvu; utusaidie, Ee BWANA, Mungu wetu; kwa kuwa sisi twakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja juu ya jamii kubwa hii. Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu wetu, asikushinde mwanadamu. 12#2 Nya 13:15 Basi, BWANA akawapiga Wakushi mbele ya Asa, na mbele ya Yuda; na Wakushi wakakimbia. 13#Mwa 10:19; 20:1; Zab 46:1-11 Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; wakawaua Wakushi wengi sana asipone hata mmoja; kwa sababu waliangamizwa mbele za BWANA, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka wengi sana. 14#Mwa 35:5; Kut 15:16; Kum 11:25; 2 Nya 17:10; 20:29 Wakaipiga miji yote kandokando ya Gerari; maana hofu ya BWANA ikawajia; nao wakaiteka nyara miji yote, kwa maana zilikuwamo ndani yake nyara nyingi mno. 15Wakazipiga pia hema za ng'ombe, wakachukua kondoo wengi na ngamia, wakarudi Yerusalemu.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 

Learn More About BIBLIA KISWAHILI