2 Mambo ya Nyakati 4
RSUVDC

2 Mambo ya Nyakati 4

4
Mapambo ya hekalu
1 # Kut 27:1; 1 Fal 9:25; 2 Fal 16:14; Eze 43:13 Tena akafanya madhabahu ya shaba, dhiraa ishirini urefu wake, na dhiraa ishirini upana wake, na dhiraa kumi kwenda juu kwake. 2#Kut 30:18; 1 Fal 7:23 Tena akaifanya bahari ya kusubu,#4:2 ‘Tangi la maji’ dhiraa kumi toka ukingo hadi ukingo, ya mviringo, na kwenda juu kwake ilikuwa dhiraa tano; na uzi wa dhiraa thelathini kuizunguka kabisa. 3#1 Fal 7:24 Na chini yake palikuwa na mifano ya fahali,#4:3 Au, maboga (1 Fal 7:24). walioizunguka pande zote, kwa dhiraa kumi, wakiizunguka pande zote ile bahari. Fahali#4:3 Tazama 4:2. walikuwa safu mbili, wakayeyushwa hapo ilipoyeyushwa hiyo bahari.#4:3 Tazama 4:2. 4Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani. 5#1 Fal 7:26 Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi#4:5 Tazama 2:10. elfu tatu, kukaa ndani yake. 6#1 Fal 7:38; Ebr 9:9 Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea. 7#1 Fal 7:49; Kut 25:31 Alivitengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu, kama vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto. 8#1 Fal 7:48 Akatengeneza na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia moja ya dhahabu. 9#1 Fal 6:36 Tena akatengeneza ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba. 10#1 Fal 7:39 Nayo bahari akaiweka upande wa kulia kwa mashariki, kuelekea kusini. 11#1 Fal 7:40 Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni.
Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu; 12#1 Fal 7:41 zile nguzo mbili, na mabakuli, na mataji mawili yaliyokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo; 13#Kut 28:33,34; 1 Fal 7:20; Wim 4:13; Yer 52:23 na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yalikuwa juu ya nguzo. 14#1 Fal 7:27,43 Akatengeneza vitako, akatengeneza na mabeseni juu ya vitako; 15mafahali kumi na wawili chini yake. 16#1 Fal 7:14,45 Vyungu, pia sepetu, nyuma na vyombo vingine vyote, Huram-abi#4:16 Au, Huramu babaye. akamtengenezea mfalme Sulemani kwa ajili ya nyumba ya BWANA, vilikuwa vya shaba iliyong'arishwa. 17#1 Fal 7:46 Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda. 18#1 Fal 7:47 Ndivyo Sulemani alivyovitengeneza vyombo hivi vikiwa vingi sana, uzani wa shaba lliyotumika haukujulikana. 19#1 Fal 7:48-50; 2 Fal 24:13; Yer 28:3; Dan 5:2,3; Kut 25:30; 1 Nya 28:16 Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho; 20#Kut 27:20,21 na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika; 21#Kut 25:31; 37:20; 1 Fal 6:18-35 na maua, na taa, na makoleo, ya dhahabu, ndiyo dhahabu bora; 22#1 Fal 6:31 na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 

Learn More About BIBLIA KISWAHILI