3Yohana UTANGULIZI
RSUVDC

3Yohana UTANGULIZI

UTANGULIZI
Waraka huu umeandikwa na Yohana ambaye anajiita “Mzee” (tazama utangulizi kwa Waraka wa Kwanza wa Yohana). Ijapokuwa Waraka huu unawekwa kwenye kundi la “Nyaraka kwa Watu Wote” inaonekana kwamba ulitumwa kwa mtu binafsi aitwaye Gayo ambaye alikuwa rafiki yake mwandishi.
Katika kanisa fulani huko Asia Ndogo alikuwapo kiongozi aliyependa kuchukua madaraka. Huyo anaitwa Diotrefe. Diotrefe alikataa kupokea waalimu na wahubiri halali waliofundisha ukweli wa Injili. Vile vile hakutaka kupokea wajumbe waliotoka kwa mtume Yohana na hivyo kumkataa Mtume Yohana mwenyewe.
Waraka unamtia moyo Gayo aliyekuwa mmoja wa viongozi katika kanisa hilo apokee na kusaidia Wakristo waliosafiri wakihubiri na kufundisha ukweli wa Injili. Anamtahadharisha Gayo kuhusu Diotrefe na kumsifu Demetrio na wengine wanaowapa msaada wahubiri wa kweli.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 

Learn More About BIBLIA KISWAHILI