Esta (Gir) F
RSUVDC

Esta (Gir) F

F
Ndoto ya Mordekai yatimizwa
4 Mordekai akasema, Mambo hayo yametoka kwa Mungu; 5 maana naikumbuka ndoto niliyoiota juu ya mambo hayo, wala hakuna neno lake lisilotimia. 6 chemchemi ndogo ilikuwa mto, kukawa na nuru na jua na maji mengi. Mto ndio Esta, aliyeolewa na mfalme akawa malkia. 7 Yale majoka ndiyo mimi na Hamani; 8 nayo mataifa ni yale yaliyokusanyika pamoja kulifuta jina la Wayahudi. 9 Na taifa langu ni Israeli, waliomlilia Mungu wakaokoka. Maana Mungu amewaokoa watu wake na kutuopoa katika maovu hayo yote. Bwana amefanya ishara kuu na mambo ya ajabu yasiyofanyika katikati ya mataifa. 10 Aliweka kura mbili, moja ya watu wake na moja ya mataifa; 11 na kura hizi mbili zilianguka katika saa na dakika na siku ya hukumu, mbele ya Mungu na mataifa yote. 12 Mungu akawakumbuka watu wake, akawapa haki urithi wake. 13 Kwa hiyo siku hizi zitaadhimishwa kwao katika mwezi Adari, siku za kumi na nne na kumi na tano za mwezi huo huo, kwa mkusanyiko wa furaha na shangwe mbele ya Mungu, kizazi kwa kizazi daima, katika watu wake Israeli.
Maelezo ya ziada
14 Katika mwaka wa nne wa utawala wa Tolemayo na Kleopatra, Dositheo, aliyesema yu kuhani na Mlawi, na Tolemayo mwanawe walikuja Misri na waraka huu wa Purimu; wakasema habari zake zi kweli, na ya kuwa Lisimako mwana wa Tolemayo, mkaaji wa Yerusalemu, alikuwa ameufasiri.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 

Learn More About BIBLIA KISWAHILI