Ezekieli 15
RSUVDC

Ezekieli 15

15
Mzabibu usiofaa
1Neno la BWANA likanijia, kusema, 2#Zab 80:8; Hos 10:1 Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni? 3Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yoyote? Watu waweza kufanya kigingi kwa huo, ili kutundika chombo chochote? 4#Yn 15:6 Tazama, watupwa motoni kuwa kuni moto unapoziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yoyote? 5Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yoyote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yoyote? 6Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu. 7#Law 17:10; Zab 34:16; Yer 21:10; 48:43,44; Isa 24:18; Amo 5:19; Eze 6:7; 7:4 Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao. 8Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 

Learn More About BIBLIA KISWAHILI