Yoshua 16
RSUVDC

Yoshua 16

16
Nchi ya Efraimu
1 # Hes 33:45 Sehemu waliyopewa wana wa Yusufu ilianza kutoka mto wa Yordani hapo Yeriko, hapo penye maji ya Yeriko upande wa mashariki, maana, ni hiyo nyika, kukwea kutoka Yeriko kati ya hiyo nchi ya vilima mpaka Betheli; 2#Mwa 28:19; Yos 18:13; Amu 1:26 kisha ikatoka huko Betheli kuendelea Luzu, kisha ikaendelea hata kuufikia mpaka wa Waarki mpaka Atarothi; 3#Yos 18:13; 21:22; 2 Nya 8:5; 1 Nya 7:28; 1 Fal 9:15 kisha ikateremkia upande wa magharibi hadi kuufikia mpaka wa Wayafleti, hadi mpaka wa Beth-horoni ya chini, hadi kufikia Gezeri; na matokeo yake yalikuwa hapo baharini. 4#Yos 17:14 Na wana wa Yusufu, Manase na Efraimu, walitwaa urithi wao. 5#Yos 18:13; 2 Nya 8:5 Na mpaka wa wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao ulikuwa hivi; mpaka na urithi wao upande wa mashariki ulikuwa ni Ataroth-adari, hata Beth-horoni wa juu; 6#Yos 17:7 kisha mpaka ukatokea kuendelea upande wa magharibi huko Mikmeta upande wa kaskazini; kisha mpaka ukazunguka kwenda upande wa mashariki hata Taanath-shilo, kisha ukaendelea upande wa mashariki wa Yanoa; 7#1 Nya 7:28 kisha uliteremka kutoka Yanoa hadi Atarothi, na Naara, kisha ukafika Yeriko, na kutokea hapo penye mto wa Yordani. 8#Yos 17:9; 19:28 Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hadi kijito cha Kana; na mwisho wake ulikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao; 9pamoja na ile miji iliyotengwa kwa ajili ya wana wa Efraimu katikati ya urithi wa hao wana wa Manase, miji yote pamoja na vijiji vyake. 10#Amu 1:29; Yos 15:63; 1 Fal 9:16,20,21; Mwa 9:25; Yos 17:12,13 Nao hawakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa Gezeri; lakini hao Wakanaani waliketi kati ya Efraimu, hata hivi leo, wakawa watumishi wa kufanya kazi za shokoa.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 

Learn More About BIBLIA KISWAHILI