6
Maono ya nane: Magari manne ya vita
1Nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, yanatokea magari ya vita manne, yanatoka kati ya milima miwili, na milima hiyo ilikuwa ni milima ya shaba. 2#Zek 1:8; Ufu 6:4,5 Katika gari la kwanza walikuwa farasi wekundu; na katika gari la pili walikuwa farasi weusi; 3#Ufu 6:2 na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu. 4#Zek 5:10 Nikajibu, nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Hawa ni nini, Bwana wangu? 5#Zab 68:17; Ebr 1:7,14; 1 Fal 22:19; Ayu 1:6; Dan 7:10; Lk 1:19; Ufu 7:1 Malaika akajibu, akaniambia, Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele za Bwana wa dunia yote. 6#Yer 1:14 Gari lile lenye farasi weusi latoka kwenda hata nchi ya kaskazini; nao farasi weupe wanatoka kwenda katika nchi ya magharibi;#6:6 Katika Kiebrania ni ‘wakatoka kufuata nyuma yao’. na wale wa rangi ya kijivujivu wakatoka kwenda hadi nchi ya kusini. 7#Mwa 13:17 Farasi wale walipotoka, walitaka kwenda huko na huko katika dunia; naye akawaambia, Haya! Tokeni, mwende huko na huko katika dunia. Basi wakaenda huko na huko katika dunia. 8#Mhu 10:4 Ndipo akaniita, akaniambia akisema, Tazama, wale waendao mpaka nchi ya kaskazini wameituliza roho yangu katika nchi ya kaskazini.
Kutawazwa kwa chipukizi
9Neno la BWANA likanijia, kusema, 10#Ezr 2:1 Pokea vitu mikononi mwa baadhi ya watu waliohamishwa, yaani, Heldai, na Tobia, na Yedaya; na siku hiyo hiyo nenda ukaingie katika nyumba ya Yosia, mwana wa Sefania, waliyoifikia kutoka Babeli; 11#Kut 28:36 naam, pokea fedha na dhahabu, ukatengeneze taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu; 12#Isa 9:6; 4:2; Zek 3:8; Mik 5:5; Mal 3:1; Yer 23:5; 33:15; Zek 13:7; 3:8; Mk 15:39; Lk 1:78; Yn 1:45; Zab 80:15-17; Mt 16:18; Efe 2:20; Flp 2:9; Ebr 2:9 ukamwambie, ukisema, BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni Chipukizi; naye atakua katika mahali pake, naye atalijenga hekalu la BWANA. 13#Zab 21:5; 110:4; Isa 22:24; Ebr 3:1 Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atakuwa na heshima ya kifalme; na ataketi na kutawala; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na maelewano yenye amani yatakuwa kati ya hao wawili. 14#Mk 14:9 Na hayo mataji yatakuwa ya Heldai, na Tobia, na Yedaya; na kwa fadhili za mwana wa Sefania; yawe kumbukumbu katika hekalu la BWANA. 15#Efe 2:13 Nao walio mbali watakuja na kusaidia kujenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu.