UTANGULIZI
Kijitabu hiki cha Nahumu kinatangaza kuteketezwa kwa Ninewi, mji mkuu wa utawala wa Ashuru. Nahumu anatabiri na kueleza kwa ufasaha sana maangamizi hayo hata anajulikana kama mmoja wa washairi maarufu wa Israeli. Kuanguka kwa Ninewi ni adhabu kutoka kwa Mungu ambaye huwaadhibu wote wanaopinga matakwa yake: 1:11; 2:1. Kitabu kinasisitiza na kutilia mkazo kwamba Mwenyezi-Mungu hauadhibu udhalimu, ukatili na maisha ovyo ya watu.