Zaburi 122
BHND

Zaburi 122

122
Sifa za Yerusalemu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1Nilifurahi waliponiambia:
“Twende nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu.”
2Sasa tuko tumesimama,
kwenye malango yako, ee Yerusalemu!
3Yerusalemu, mji uliojengwa,
ili jumuiya ikutane humo.#122:3 mji uliojengwa ili jumuiya ikutane humo: Tafsiri nyingine: Uliojengwa kwa mpango mzuri na umetengemaa. Kiebrania si dhahiri.
4Humo ndimo makabila yanamofika,
naam, makabila ya Israeli,
kumshukuru Mwenyezi-Mungu kama alivyoagiza.
5Humo mmewekwa mahakama ya hukumu ya haki,
mahakama ya ukoo wa kifalme wa Daudi.
6Uombeeni Yerusalemu amani:
“Wote wakupendao na wafanikiwe!
7Ndani ya kuta zako kuwe na amani,
majumbani mwako kuweko usalama!”
8Kwa ajili ya jamaa na ndugu zangu,
ee Yerusalemu, nakutakia amani!
9Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,
ninakuombea upate fanaka!
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.Learn More About Biblia Habari Njema