UTANGULIZI
Tofauti sana na vitabu vingine vya manabii, kitabu cha Yona ni simulizi. Kinasimulia habari za nabii mmoja ambaye anatajwa mara moja tu katika A.K. katika (2Fal 14:25). Yona anajaribu kwanza kukwepa wito wa Mungu na baadaye ananung'unika kwamba alipofuata wito huo wa kwenda kuhubiri, yalipatikana mafanikio ambayo hakuyatazamia. Waninewi walitubu, naye Yona hakupendezwa. Fundisho kubwa: Mungu mwenyewe anaongoza wasemaji wake bila ya wao kutaka. Pili: Binadamu hawezi kumwekea Mungu mipaka ya upendo wake kwa watu wake.